Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Abdulimalik Mollel, akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani)
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Kampuni ya Global Education Link
(GEL) kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Wizara ya
Elimu na Ufundi pamoja na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania
(Tantrade) wameandaa maonyesho ya kwanza ya kimataifa ya elimu (TIEE)
yanayotarajiwa kufanyika Disemba 17 hadi 21 mwaka huu katika viwanja
vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Global link Education, Abdulmalik Mollel,
alisema lengo la maonyesho hayo ni kutambulisha wadau wa elimu kwa
pamoja ili kuweza kutoa huduma ya pamoja kwa wananchi na kuwaelimisha
juu ya mambo muhimu yaliyopo katika kila sekta.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Tred), Jacqueline Mneney, akizungumza jambo.
Alisema ushiriki wa asasi
mbalimbali kwa kushirikiana na sekta binafsi utakuwa na chachu ya
mabadiliko ya elimu kwa kupitia mpango wa matokeo makubwa sasa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney, alisema
wakati umefika kwa Watanzania kujua umuhimu wa maonyesho ya Elimu maana
yamekuja kutatua matatizo mbali mbali waliyokuwa wakiyapata wazazi pindi
wanapokuwa wanawatafutia shule na vyuo watoto wao.
Aidha alisema maonyesho hayo
yataleta manufaa makubwa na changamoto chanya hasa katika kuongeza
ushindani katika sekta ya elimu ambayo itasaidia mpango wa matokeo
makubwa sasa.
Maonesho hayo yanatarajiwa kupata washiriki zaidi ya 500 na wananchi mbalimbali zaidi ya 350,000 kutoka ndani na nje ya nchi.
Kauli mbiu ya maonesho hayo ni ‘KUWEKA JITIHADA ZA PAMOJA KATIKA KUBORESHA MFUMO WA ELIMU TANZANIA NI NJIA THABITI YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU KATIKA TAIFA.’
EmoticonEmoticon