Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, CCM,
anayewakilisha Lindi Mjini, Mama Salma Kikwete akisalimiana na viongozi
wa Kata ya Mtandi iliyoko Lindi Mjini wakati alipotembelea Kata hiyo kwa
ajili ya kufanya mkutano wa kampeni katika uchaguzi wa viongozi wa
serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini kote tarehe 14.12.2014.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha Lindi mjini na Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akionyesha ishara ya vidole viwili kuashiria kuunga
mkono pendekezo la muundo wa serikali mbili nchini wakati alipozungumza
na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Kata ya Mtandi tarehe 5.12.2014.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha wilaya ya Lindi Mjini na Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi
wa Kata ya Mtandi katika mkutano uliofanyika katika Mtaa wa Maisara kwa
ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini unaotarajiwa
kufanyika tarehe 14.12.2014.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM anayewakilisha wilaya ya Lindi Mjini na Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa Chama Cha Mapinduzi
wa Kata ya Mtandi katika mkutano uliofanyika katika Mtaa wa Maisara kwa
ajili ya uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa nchini unaotarajiwa
kufanyika tarehe 14.12.2014.
Mama Salma Kikwete, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi
anayewakilisha Lindi Mjini akishiriki kucheza na baadaye kuwahutubia
wananchi wa Kata ya Mwenge huko Lindi Mjini wakati akishiriki kuwapigia
kampeni za uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa
kufanyika nchini kote tarehe 14.12.2014.
Baada
ya kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye Kata ya Mwenge huko Lindi Mjini
Mama Salma Kikwete anaonekana akimbeba mtoto Juma Selemani ambaye naye
alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria mkutano wa kampeni.
…………………………………………………..
Na Anna Nkinda – Lindi
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) wilaya ya Lindi mjini wametakiwa kutokubali kurubuniwa kwa kitu
chochote kile ili wawapigie kura wagombea wa vyama vya upinzani bali
waungane kwa pamoja katika kampeni na kuhakikisha chama hicho kinapata
ushindi wa kishindo.
Mwito huo umetolewa jana na
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia wilaya ya Lindi
mjini Mama Salma Kikwete wakati akiwanadi kwa wananchi wagombea wa
chama hicho wanaowania nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa Wenyeviti na
Wajumbe wa Serikali za Mitaa katika Kata ya Mwenge.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema lengo la chama chochote cha Siasa ni
kushika Dola kuanzia ngazi ya mtaa hadi Taifa hivyo basi wanachama
hao wasikubali kurubuniwa bali waendelee kukitetea na kukipigania Chama
chao ili kipate ushindi katika mitaa yote 117 ya Kata hiyo.
“Viongozi wanaogombea tena
wamechaguliwa kutokana na kazi yao nzuri. Nanyi ambao kura zeu
hazikutosha wakati wa mchakato wa kuchagua msilaumu, bali muwapiganie
wagombea wote na kuhakikisha wanashinda angalieni maslahi ya chama
kwanza mambo binafsi baadaye”, alisema Mama Kikwete.
Aidha Mama Kikwete aliwaomba
wananchi wa wilaya hiyo kutumia maarifa na ujuzi waliopewa na Mwenyezi
Mungu wa kutambua mema na mabaya na kutokubali kudanganywa na kundi la
watu wachache ili waipoteze amani yao.
Mama Kikwete alisema, “Wenzenu
wamepiga hatua kubwa za maendeleo katika mikoa yao huku Lindi Mwenyezi
Mungu katupa neema maendeleo yanakuja sasa. Wanakuja huku kuwadanganya
ili mfanye vurugu na kurudisha maendeleo yenu nyumba, msifuate mkumbo na
kuchezea amani kwani vurugu zinarudisha nyuma maendeleo”.
Aliwasihi wananchi waliohudhuria
mkutano huo kuhakikisha watoto wao wanaenda shule ili wapate viongozi
wazuri wa baadaye ambao watawaletea maendeleo kwani bila ya kuwa na
elimu ni vigumu kupata maendeleo.
MNEC huyo pia aliwashukuru wanaume
waliowaruhusu wake zao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na
kuwapongeza wanawake kwa kutokukubali kubaki nyuma na kuomba kugombea
nafasi hizo.
Mama Kikwete yupo wilayani humo
kwa ajili ya shughuli za kichama ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye
kampeni na kuwanadi wagombea wa chama hicho wanaowania nafasi mbalimbali
za uongozi katika uchaguzi wa viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na
Vitongoji utakaofanyika tarehe 14 mwezi huu.
EmoticonEmoticon