!
Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya ambaye ni mrithi wa kazi za
marehemu Shehe Yahya amesema kuwa, penzi la mastaa wa Kibongo,Wema
Sepetu na Nasibu Abdul ‘Diamond’ bado halijafika mwisho, watarudiana na
kufunga ndoa. Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Akizungumzia penzi la wawili hao ambao siku chache zilizopita
wameripotiwa kumwagana alisema, hali hiyo ni ya mpito tu haimaanishi
kuwa hiyo ndiyo tamati ya mapenzi yao, sababu nyota zao zinategemeana
japo ya Wema ina nguvu kubwa kuibeba ya Diamond.Staa
wa Bongo Movies, Wema Sepetu. “Msifikiri kwamba penzi lao ndiyo
limefika mwisho, hakuna kitu kama hicho ni mara ngapi wameachana na
kurudiana hata hili la sasa natabiri watarudiana,” alisema Malim.
EmoticonEmoticon