KAGERA YACHARAZWA BAKORA HADHARANI.

September 20, 2014


NA SAFARI CHUWA,TANGA.

TIMU ya Maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa mkoani Tanga leo wameanza vema michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kuibamiza Kagera Sugar bao 1-0,mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani.
 
Mchezo ambao ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa zamu ambapo Mgambo shooting walianza kucheza kwa umakini mkubwa ambao uliwawezesha kufanikiwa kaundika bao la kwenye dakika ya 14 likifungwa na Ramadhani Pera aliyepiga mpira umbali wa mita 40 na kumshinda mlinda mlango wa Kagera Agatony Anthony  na kutinga wavuni.


Baada ya bao hilo Mgambo waliweza kuendeleza wimbi la mashmbulizi langoni mwa Kagera lakini bahati ya mabao ilikuwa sio yao kutokana na wachezaji wake kupata nafasi za wazi na ksuhindwa kuzifanyia kazi.

Mpaka timu zote zinakwenda mapumziko matokeo yalisomeka 1-0 ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa timu zote baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi ya wachezaji wake lakini hali haikuweza kubadilika.


Bila shaka Kagera wanapswa kujilaumu kutokana na kutokuwa makini kwenye mechi hiyo hali iliyopelekea kukosa penati ya wazi dakika ya 36 kupitia Abubakari Mtiro baada ya mchezaji wa Mgambo shooting Mohamed Nampokwa kuunawa mpira eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Kenedy Mapunda kutoka dar kuamuru penati.


Ki ujumla mgambo waliweza kuutawala mchezo huo kwa kucheza vema kuanzia mwanzo mpaka mwisho jambo ambalo linaonyesha maandalizi mazuri yaliyoyafanya kuelekea mechi hiyo.

Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »