Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye wakiwasalimia wakazi wa Kibaha mjini wakati
wakiwasili kwenye uwanja wa mkutano .
Kikundi
cha ngoma cha Kisamamwe kikitumbuiza ngoma ya Afrika kabla ya kuanza
kwa mkutano wa hadhara ambapo Katibu Mkuu wa CCM alihutubia wananchi wa
Kibaha mjini.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibaha mjini
ambapo aliwaambia wapinzani wamekosa hoja ya msingi kiasi cha kuamua
kufanya maandamano ya kuleta vurugu nchini.
Sehemu ya Umati wa watu wakisikiliza mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Wana CCM wakiwa kwenye mkutano
Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Francis Koka akihutubia wakazi wake na kuwaambia kuwa pamoja na jitihada zote anazofanya maji bado ni donda sugu ila ufumbuzi upo njiani.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibaha mjini
wakati wa mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia viongozi wa halmashauri
hawana budi kukaa na wafanya biashara ndogo ndogo kujadili kodi kabla ya
kuwapangia kuona kama wana uwezo wa kulipa ama hapana hii itasaidia
kupunguza lawama na mikingamo baina ya wafanya biashara na halmashauri.
EmoticonEmoticon