WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII AZINDUA BODI MPYA YA USHAURI WA UONGOZI WA HOSPITALI BINAFSI NCHINI

September 20, 2014


                                                                Dotto Mwaibale

SERIKALI imesema itaainisha ukomo wa tozo kwa kila huduma inayotolewa kwa kila ngazi ya kituo cha huduma ili kudhibiti gharama za huduma za afya nchini.

Kauli hiyo ilitolewa  na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid Dar es Salaam wakati akizindua bodi mpya ya ushauri ya Hospitali binafsi nchini.

Dk. Rashid alisema hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kuhusu huduma zinazotolewa na hospitali hizo hivyo hatua hiyo itasaidia kuboresha mfumo na kuwatendea haki wananchi wanaotumia vituo  vya kutolea huduma za afya.

"Malalamiko haya ni pamoja na huduma zisizo na ubora unaotakiwa na gharama zinazotolewa kwa huduma hizo .Sheria iliyopo inatutaka kudhibiti bei ya huduma hizi kwa kuzingatia malalamiko haya pamoja na matakwa ya sheria yenyewe," alisema Dk. Rashid.

Hata hivyo alibainisha kuwa licha ya kuwepo wa changamoto hizo huduma zinazotolewa na hospitali za watu binafsi zimechangia katika mafanikio  yaliyopatikana katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Kuhusu bodi hiyo Dk .Rashid aliwataka wajumbe wapya wa bodi hiyo kufanya vikao vya mara kwa mara vinavyolenga uboreshwaji wa utoaji wa huduma.Na kuwataka kuendeleza utaratibu wa kusajili vituo vipya na kufupisha usajili kwa kutmia muda mfupi  kwa kutumia mfumo wa kielektroniki.

Alibainisha kuwa wajumbe wa bodi ya awali iliyosimamiwa na Mwenyekiti Dk. Deo Mtasiwa imesaidia kuboresha uwajibikaji wa wahusika hivyo kuboresha huduma na imeokoa maisha ya wananchi wengi ambayo yangekuwa hatarini endapo bodi isingetekeleza majukumu yake ipasavyo.

Alitaja wajumbe wa bodi mpya kuwa ni Dk.Donan Mbando ambaye ni Mwenyekiti, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa mbeya Dk. Mpoki Ulisubisya, Mkurugenzi wa Hospitali ya Bugando Profesa Chalres Majinge, Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi (NHIF), DK. Frank Lekey.


Wajumbe wengine ni Mkurugenzi Msaidizi- Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba Dk. Sijenunu Aaron, Mkurugenzi wa Association of Private Health Facilities (APHTA), Mwakilishi wa Mkurugenzi, Christian Social Services Comission (CSSC), Dk.Jane Kahabi na Mwanasheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Onorious Njole.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo iliyomaliza muda wake na mpya wakati akizindua bodi hiyo Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa bodi mpya, Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey  akitoa neno la shukurani. Kushoto ni Naibu Msajili Hospitali Binafsi Dk.Mahewa Lusinde na Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Mpoki Ulisubisya.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),akimkabidhi cheti cha utumishi wa bodi hiyo,Profesa Bakari Lembariti. Katikati ni Mganga Mkuu wa Serikali, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dk.Donan Mmbando. Vyeti hiyo walitunukiwa wajumbe wote waliomaliza muda wao.
 Wajumbe wa Bodi mpya wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tiba na Masuala ya Kiufundi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Dk.Frank Lekey, Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Dk.Mpoki Ulisubisya, Mwanasheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Onorius Njole, Mkurugenzi Association of Private Health Facilities-APHTA na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi-Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba, Dk.Sijenunu Aaron.
 Wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake. Kutoka kulia ni Profesa .Bakari Lembariti, Profesa Charles Majinge, Dk.Edda Vahahula, Dk.Jane Kahabi na Dk.Eliuter Samky.
 Mkutano ukiendelea.
 Mkurugenzi wa Tiba wa Wizara hiyo, Dk.Margareth Mhando na Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki na Ubora, Dk.Mohamed wakiwa kwenye mkutano huo.
 Katibu wa Bodi hiyo, Dk.Pamella Sawa akizungumza katika mkutano huo.
 Kaimu Mkurugenzi Msaidizi-Hospitali za Umma na Binafsi Idara ya Tiba, Dk.Sijenunu Aaron akiteta jambo na Mkurugenzi Msaidizi wa Vituo vya Umama na Binafsi na Mwakilishi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali Binafsi Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Ruth Suza.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »