Waliosababishia Serikali hasara ya bn 40/- kukiona
Naibu Waziri wa Fedha, Mungulu Nchemba
Agizo hilo lilitolewa na Naibu
Waziri wa Fedha, Mungulu Nchemba, akisema wakuu hao pamoja na waajiri
wametumia mwanya wa wafanyakazi wao katika ubadhirifu wa fedha kwa
maslahi yao binafsi.
Kadhalika, wizara inawataka
maafisa utumishi na waajiri kuhakiki upya taarifa wanazoweka katika
mfumo ni sahihi ili watumishi wao wawekewe malipo yao katika akaunti kwa
wakati mwafaka.
“Zoezi hili ni endelevu, hivyo
tumebaini tatizo na tunatafuta njia ya kulimaliza na hii tuliyowaagiza
waajiri itakuwa njia ya kutokea, hivyo tutalinganisha taarifa zao na
muda wa watumishi wao tuone tatizo lilikuwa wapi,” alisema.
Pia, alisema hakuna sababu ya
wizara kuendelea kulipa malipo hewa wakati kuna kundi la wafanyakazi
katika taasisi na mashirika hayo, ambao kazi yao ni kuhakiki mafaili na
wanalipwa mishahara mikubwa huku wale wanaojituma wakiendelea kujaziwa
mishahara hewa.
Aliwaagiza waajiri na maafisa hao
kufikisha orodha ya majina ya watumishi wakiambatanisha na taarifa
sahihi ya mishahara tarehe za mwanzo za kila mwezi zifanyiwe kazi mapema
ili kuwepo na uwajibikaji katika sehemu za kazi.
Alisema fedha za miradi katika
taasisi hizo zitatolewa kulingana na mchanganuo wa malipo yao, “Hatuwezi
kuendelea kutoa malipo hewa kinyemela tena, hivyo wataalamu wetu
watashirikiana na wakuu hao wa maradi kuangalia kama unakidhi
kutekelezewa,” alisema.
EmoticonEmoticon