Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akiwasili kwenye makao makuu ya Jeshi
la Polisi nchini,Mapema leo asubuhi tayari kwa kwenda kuhojiwa juu kauli
aliyoitoa kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho hivi katibuni,kuwa
watafanya maandamano nchini nzima bila kikomo.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema,Prof.
Abdallah Safari na Wakili wa Chama,Wakili Mabele Marando wakiwasili
kwenye Makao Makuu wa Jeshi la Polisi mapema leo.
Baadhi ya wapenzi na wanachama wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakishangilia baada ya gari
lililokuwa limembeba Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe,
alipowasili leo Makao Makuu wa Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, kwa
mahojiano.
Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA John
Mnyika akizungumza na waandishi wa habari waliokuwepo kwenye eneo la
makao makuu ya Jeshi la Polisi,juu ya kile kilichokuwa kikiendelea
kwenye mahojiani katika ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Jeshi la Polisi.
Mwenyekiti wa Chama cha DP, Christopher
Mtikila akihojiwa na askari Polisi, alipowasili Makao Makuu ya Polisi
jijini Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa bajaji, ambako Mwenyekiti wa
CHADEMA, Freeman Mbowe alihojiwa na Polisi.
EmoticonEmoticon