Na Magreth Kinabo, Dodoma
26/08/2014.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Namba Tatu
ya Bunge hilo, Dkt. Francis Michael ametoa ufafanuzi kuhusu suala la
utungaji wa Katiba ambalo hufanyika kwa mifumo miwili, na kuwataka
wananchi wasipotoshwe na mfumo unaotumika.
Kauli
hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti huyo, ambaye pia ni mtaalam wa sheria
wakati akizungumza katika kipindi cha Jambo kinachorushwa na Shirika
la Utangazaji Tanzania (TBC).
Akifafanua
kukuhusu mifumo hiyo, amema kuwa kuna mfumo wa kwanza ,ambao hutumia
Tume kama ilivyokuwa Tume ya Jaji Joseph Warioba yenye watu ambayo
ilikuwa na kazi ya kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi na
kutengeneza Rasimu ya Katiba Mpya , baadaye Bunge Maalum la Katiba
linapitia maoni ya Rasimu hiyo, ambapo kwa mujibu wa Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2014 linaweza kubadilisha na kuongeza kwa
ajili ya kuiboresha.
“Katika
mfumo huu lazima Bunge liwepo kwa ajili ya kuiboresha kabla ya kwenda
kupigiwa kura na wananchi,” alisema Dkt. Michael .
Dkt.
Michael aliutaja mfumo wa pili ni ule wa kutumia Tume Maalum ya
Wataalam, ambao wanawajibu wa kuandika Katiba na hakuna chombo chochote
kitakachokuwa na wajibu wa kuibadilisha, bali itakwenda moja kwa moja
kwa wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura.
“Wananchi wasichanganywe na mfumo unaotumika,” alisisitiza Dkt. Michael.
Akizungumzia
kuhusu uwasilishaji wa nyongeza ya mapendekezo yaliyowasilishwa na
makundi mbalimbali hivi karibuni kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la
Katiba, Mhe. Samuel Sitta yamepokelewa kwa mujibu wa sheria hiyo,
kipengele cha 25 ambapo Bunge hilo lina nguvu kufanya marekebisho au
kuongoza vifungu vingine pale linapoona inafaa.
Aidha,
Dkt. Michael amefafanua kuwa wanatumia nafasi hiyo kisheria na
kikanuni, kupokea nyongeza ya mapendekezo hayo kutoka kwa watu
mbalimbali.
Akizungumzia
kuhusu suala hilo, Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhe, Ridhiwani Kikwete
alisema linafanyika kisheria hivyo mtu au kikundi kinaweza kuwasilisha
mapendekezo ya nyongeza.
Mhe,
Ridhiwani alisema nyongeza ya mapendekezo hayo, uwasilishwa kwenye
Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo, ambayo nayo hupeleka kwa Kamati 12 za
Bunge hilo kwa ajili ya kuratibu mambo ya msingi na kuyachukua .
Aliongeza
kuwa suala hilo pia linaweza kufanyika wakati wa mjadala wa Bunge
hilo,mjumbe anaweza kulishawishi Bunge hilo, kwa kuwa sheria , kanuni
na miongozo inaruhusu.
EmoticonEmoticon