HATIMAYE
yametimia. Wakati mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward
aliposema kuwa watavunja rekodi ya usajili England msimu huu, ilionekana
kama masihara lakini sasa ukweli umedhihirika.
Angel
di Maria tayari ametua Manchester United kwaajili ya mazungumzo binafsi
pamoja na vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili wake wa pauni
milioni 60 utakaomwingizia mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki.
Di
Maria ameonekana kwenye gari akiwa ameketi kiti cha nyuma akielekea
kwenye uwanja wa mazoezi wa United kwaajili ya kwenda kukamilisha
usajili wake.
Mshambuliaji
huyo atakuwa mchezaji wa pili kwa kulipwa pesa nyingi zaidi Manchester
United akitanguliwa na Wayne Rooney na akiwa amemzidi kidogo Robin van
Persie.
EmoticonEmoticon