KAMA
Liverpool wanadhani wana ubavu wa kupimana nguvu na mabingwa watetezi
wa Ligi Kuu ya England, Manchester City basi wakajipange upya.
Liverpool
inayojinasibu kusaka ubingwa wa Ligi Kuu, imejikuta ikiambulia kipigo
cha 3-1 kutoka kwa Manchester City kwenye uwanja wa Etihad Jumatatu
usiku.
Ikishuhudiwa
na mchezaji wao mpya Mario Balotteli aliyekuwa jukwaani kufuatilia
mchezo huo, Liverpool ikakukuruka hadi dakika ya 41 kabla ya kuruhusu
bao la kwanza lilifungwa na Stevan Jovetic aliyekuwa nyota wa mchezo.
Dakika
ya 55, kwa mara nyingine tena Jovetic akawafanya Liverpool waende
nyavuni kuokota mpira baada ya kufunga tamu lililotokana na pasi 19.
Zilikuwa
ni gonga za aina yake ambapo ukingoni mwa gonga hizo Stevan Jovetic
alimpa pande Samir Nasir na kukimbia mbele kusubiri arudishiwe mpira na
Nasiri na ndivyo ilivyokuwa – akarudishiwa mpira na kumtungua kipa Mignolet, mashabiki wa City wakaingia wazimu.
Sergio Aguero aliyeingia dakika ya 69 kuchukua nafasi za Dzeko akaipatia City bao tatu sekunde chache tu baada ya kuingia uwanjani.
Liverpool,
timu ya pili duniani kwa kumwaga pesa nyingi kwenye usajili msimu huu,
ikasubiri hadi dakika ya 83 kupata goli la zawadi kutoka kwa beki wa
City, Zabaleta aliyejifunga mwenyewe.
EmoticonEmoticon