Baadhi
ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa
za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo
umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es
Salaam.Mjane
wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca
Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya
kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote
zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za
kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Mjane
wa Hayati Nelson Mandela na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust
(GMT), Bi. Graca Michel akimbusu mmoja ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa
Mara kuonesha ishara ya upendo katika uzinduzi huo
Mjane
wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca
Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akisalimiana na baadhi ya viongozi
mbalimbali kutoka mkoani Mara.Baadhi
ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara wakizungumzia namna
walivyonusurika kufanyiwa vitendo vya kikatili (kukeketwa). Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka akiwasikiliza.Viongozi
mbalimbali wastaafu wa Serikali, viongozi wa dini Mkoa wa Mara,
wawakilishi wa wanafunzi Mkoa wa Mara wakiwa katika hafla ya uzinduzi
rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike
zitakazoendeshwa mkoani Mara.Baadhi
ya viongozi wa mashirika mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa
kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa
mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca
Michel leo jijini Dar es Salaam.Mjane
wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca
Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akizungumza kabla ya
kuzindua rasmi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike
zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Baadhi
ya wanafunzi wakiangalia ujumbe mfupi uliotumwa kwa simu zote
zilizosajiliwa kwa njia ya simu za kiganjani na Mjane wa Hayati Nelson
Mandela, Bi. Graca Michel kwa kushirikiana na Waziri wa Maendeleo ya
Jamii Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba kupinga ndoa za utotoni kwa
watoto wa kike.Baadhi ya wanafunzi wakitumbuiza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike.
Moja
ya kikundi cha maigizo kikionesha igizo namna mtoto wa kike
anavyokabiliana na changamoto za unyanyasaji kutoka kwa jamii katika
hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto
wa kike
JUMLA
ya wasichana wenye umri mdogo wapatao 984 wameolewa na kukatishwa
masomo huku wasichana wengine 1,628 wakikeketwa wilayani Tarime, Mkoa wa
Mara ikiwa ni miongoni mwa vitendo vya kikatili ambavyo amekuwa
akifanyiwa mtoto wa kike baadhi ya maeneo nchini Tanzania.
Takwimu
hizo za vitendo vya kikatili dhidi ya mtoto wa kike wilayani Tarime
zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John
Henjewele kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara kwenye hafla ya
uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike
zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Akizungumza
kabla ya uzinduzi wa kampeni hiyo, Henjewele alisema takwimu hizo
zavitendo vya kikatili Mkoani Mara ni za kuanzia mwaka 2013 hadi Juni
2014. Alisema baadhi ya familia eneo hilo wanamchukulia mtoto wa kike
kama kitega uchumi hivyo wamekuwa wakiwaozesha mapema ili kupata mali
(yaani ng'ombe) jambo ambalo bado uongozi wa mkoa huo kwa kushirikiana
na wadau anuai wamekuwa wakipinga na kupambana na ukatili huo.
"...Matukio
ya vitendo vya unyanyasaji kwa mtoto wa kike kwa mwaka 2013 hadi Juni
2014 ni kama ifuatavyo; watoto wa kike wapatao 984 waliozeshwa,
wasichana 1,628 walikeketwa, jumla ya wanafunzi wa kike 4,134 walipewa
mimba na kukatishwa masomo yao huku wasichana 1,912 wakifanyiwa ukatili
wa vipigo kwenye familia ama kwenye ndoa na jumla ya watoto 11
walibakwa...," alisema Henjewele.
Aidha
alisema vitendo hivyo vya kikatili kwa mtoto wa kike vinachangiwa na
baadhi ya jamii mkoani humo kuendeleza mila na desturi zilizopitwa na
wakati, migogoro ya koo, mwamko duni wa elimu kwa jamii na usiri mkubwa
wa kutokubali mabadiliko dhidi ya vitendo vya kikatili kwa jamii hiyo.
Akizungumzia jitihada zinazofanywa na viongozi wilayani hapo kukabiliana
na vitendo hivyo, alisema wamekuwa wakiendesha semina na vikao
mbalimbali na wazee wa kimila, mangariba na jamii kwa ujumla kwa lengo
la kutokomeza vitendo vya Ukatili wa kijinsia, ukeketaji pamoja na mila
na desturi zilizopitwa na wakati.
Kwa
Upande wake mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel akizungumza kabla ya
kuzindua rasmi kapeni hizo alisema viongozi kwa kushirikiana na
wanajamii mkoani Mara wakiamua kwa dhati wanaweza kukabiliana na ndoa za
utotoni na vitendo vingine vya kikatili eneo hilo.
Akizungumzia
kwa ujumla alisema jamii nyingi ya kiafrika bado zinamthamini mtoto wa
kiume zaidi ya yule wa kike ilhali watoto wote wanapaswa kuwa na haki
sawa. Aliwataka wazazi wenye mawazo kama hayo kubadilika na kutoa haki
sawa kwa watoto bila ubaguzi. Alishauri suala la uamuzi dhidi ya maisha
ya mtoto lifanywe kwa ushirikiano kwa familia nzima pamoja na
kushirikishwa mtoto.
"...Lazima
tukubali kubadilika, umefika wakati suala la uamuzi wa wakati gani wa
kuolewa kwa mtoto wa kike ufanywe kwa ushirikiano kati ya wazazi wote
pamoja na mtoto mwenyewe tena kwa wakati muafaka...lazima turejeshe
maamuzi pia kwa mtoto mwenyewe si kutumia nguvu kwa kila kitu," alisema
Bi. Michel.
Aliongeza
hata hivyo ipo haja ya kuwa na asasi za ushauri ngazi ya familia ambazo
zitakuwa zikitoa ushauri juu ya masuala ya familia kwa kuzingatia
sheria na taratibu zinazotambulika. Alisisitiza katika kampeni za sasa
juhudi na elimu ya kutosha itolewe kwa jamii mkoani Mara ili baadaye
ifanyike tathmini kwa eneo hilo jambo ambalo linaweza kusaidia mapambano
maeneo mengine hapo baadaye.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Nsoka akifafanua juu ya shughuli
za kampeni hizo alibainisha kuwa zitaambatana na utoaji elimu kwa
makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, watendaji wa vyombo
vinavyosimamia sheria, viongozi wa jamii na jamii kwa ujumla juu ya
mapambano ya kampeni hizo. Kampeni hizo baadaye zitaendelea katika
maeneo mengine ya Tanzania.
Programu
ya kampeni hiyo imefanikishwa kwa kushirikiana na Serikali, Shirika la
Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Chama cha Wanahabari Wanawake
(TAMWA), Shirika lisilo la Kiserikali la Children's Dignity Forum
(CDF), Graca Machel Trust (GMT), asasi za mkoani Mara na uongozi wa
mkoa.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
EmoticonEmoticon