Na John Walter-Manyara
Mkuu wa wilaya ya Hanang' Janeth Mayanja amewataka wananchi kujenga tabia ya vivutio vilivyopo ikiwemo kupanda mlima Hanang' unaopatikana katika wilaya hiyo mkoani manyara.
Ameyasema hayo wakati aliposhiriki katika zoezi la kupanda mlima huo, zoezi lililoandaliwa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Hifadhi ya mazingira ya Mlima Hanang' ambapo amesema zoezi hilo litasaidia vijana kujifunza,kutunza na kulinda mazingira hasa katika hifadhi hiyo.
Aidha Mayanja ametoa vyeti Kwa vijana zaidi 550 kutoka katika maeneo mbalimbali ya Mkoa Manyara ambao wamepanda mlima huo ambao ni wa nne kwa urefu nchini na kuwataka kuwa mabalozi wazuri wa kutunza na kulinda mazingira katika hifadhi hiyo.
Kwa upande wake Afisa Utalii Katika hifadhi ya Mazingira ya Mlima Hanang' Elizabeth Mbunda, amesema kutokana na juhudi mbalimbli za serikali kwa Kushirikiana na wakala wa Misitu Tanzania kuwahimiza na kuona umuhimu wa kutembelea hifadhi, muitikio wa wananchi umekuwa mkubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Mbunda amesema wenyeji wanaouzunguka mlima huo walikuwa wanauona ni kama pori la kawaida lakini baada ya Serikali kuboresha Miundombinu na na kupewa elimu na hamasa Sasa wamekuwa mabalozi wakubwa.
Ameongeza kuwa hifadhi ya mlima Hanang ni zaidi ya Utalii wa Ikolojia ya Mazingira kwani Kuna mimea inayopatikana katika hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na kinyonga anayepatikana mlima huo pekee.
Amesema zoezi hilo la kupanda mlima hufanyika Kila mwaka ifikapo tarehe 14 October siku ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere, lakini mwaka huu hawakuweza kufanya tarehe hiyo kutokana na tukio kubwa la kuzima mwenge wa Uhuru kitaifa kufanya mkoani humo.
Aidha amewatoa hofu wazawa juu ya gharama za kupanda mlima na kuona vivutio mbalimbali kwa kuwa ni rafiki na kila mmoja anaweza kumudu.
EmoticonEmoticon