KILO 7971953 ZA KOROSHO GHAFI ZAUZWA MNADA WA KWANZA RUNALI

October 23, 2023

 

Mwenyekiti wa cha RUNALI Odasi Mpunga akiongea wakati wa zoezi la Mnada wa korosho unaondeshwa na chama cha RUNALI Kwa mara ya kwanza Kwa msimu mpya wa korosho na Bei ya juu kufikia shilingi 2030. Picha na Fredy Mgunda
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akifuatilia kwa karibu Mnada wa kwanza wa zao la korosho unaoendeshwa na chama cha RUNALI


Na Ahmad Mmow, Nachingwea. 

 Jumla ya kilo 7,971,953 za korosho ghafi zimeuzwa na chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kilichopo mkoani Lindi. 

 Katika mnada huo wa kwanza kwa chama hicho, uliofanyika Oktoba 22,2023 msimu wa 2023/ 2024 bei ya juu ilikuwa shilingi 2,032 na bei ya chini shilingi 1,965 kwa kila kilo moja.  

 Kwenye mnada huo barua 43 za maombi ya kununua korosho hizo ambazo zipo katika maghala saba yaliyopo katika wilaya za Liwale, Ruangwa na Nachingwea. 

Kwa mujibu wa meneja mkuu wa RUNALI, Jahida Hassan ghala la halmashauri ya wilaya ya Nachingwea lenye kilo 1,979,396 bei ya juu katika ghala hilo ni shilingi 2,023 na bei ya chini shilingi 2,010 kila kilo moja. ¥ Alisema  ghala la Export lenye kilo 1,391,929 zimenunuliwa kwa bei ya juu ya shilingi 2023 na bei ya chini shilingi 2,010 kila kilo moja. 

Ambapo katika ghala la Lindi farmers lenye kilo 891,939  bei ya juu shilingi 2,020 na bei ya chini shilingi 2010. ¥ Meneja huyo alilitaja ghala la Lipande lenye kilo 1,369,329  bei ya juu ni shilingi  2,023 na bei ya chini ni shilingi 2,010. Huku akilitaja ghala la RUNALI lenye kilo 232,810 zilinunuliwa kwa bei moja ya  shilingi 2,023. 

Jahida alisema ghala la Umoja lenye kilo 1,40740 bei ya juu ni shilingi 2,000 na bei ya chini shilingi 1,965. 

 " Katika ghala la Hassan Mpako kuna kilo 1,650,810 korosho zake zimenunuliwa kwa bei ya juu ya shilingi 2,000 na bei ya chini 1,975.  

 Aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mnada huo uliofanyika katika viwanja vyo ofisi kuu ya RUNALI mjini Nachingwea, mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Mohamed Moyo aliwataka wanunuzi kulipia haraka mizigo yao. Huku akiwakumbusha viongozi na watendaji wa chama kikuu hicho kuharakisha malipo ya wakulima. Kwani hataki kusikia malalamiko kuhusu malipo ya wakulima. ¥ 

Aidha Moyo aliwaonya wakulima wenye tabia ya kuwa amini watu wasio watumishi wa benki kuwatolea fedha kwenye akaunti zao waache tabia hiyo. Kwani baadhi ya wakulima waliibiwa katika misimu ya mauzo ya ufuta na mbaazi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »