Wiki Ya Azaki Kuwatambua Wanawake Vijijini

October 23, 2023

 Na Jane Edward, Arusha


Wanawake wa vijijini wanatajwa kuwa  na mchango mkubwa katika maendeleo ya teknolojia kwa maeneo mbalimbali ikiwemo kupitia simu za kijangani kama wakipewa elimu ya Matumizi mazuri ya tekno.

Hayo yamesemwa Jijini Arusha na Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki za Azaki, Nesia Mahenge amesema katika kasi ya maendeleo ya teknolojia nchini lazima yamguse mwanamke, ambaye ndiye mzalishaji wa kila kitu ikiwemo kilimo.

Amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni Teknolojia na Jamii, ambapo wataangalia katika masuala ya teknolojia wapi walipotoka na wanapokwenda.

Amesema malengo ya mkutano huo ni kuimarisha uhusiano kati ya serikali na sekta binafsi, ikiwemo kuweka mikakati ya Azaki katika kutekeleza miradi kupitia teknolojia.

“Hivi sasa teknolojia inakua kwa kasi ikiwemo mabadiliko ya kidigitali, ambayo yana uwezo wa kuleta maendeleo mengi zaidi jumuishi,” amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk,Anna Henga amesisitiza wadau hao watajadili masuala ya sheria ikiwemo haki ya kumlinda mwanamke katika kujikwamua kiuchumi.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »