Mkuu
wa Wilaya Mhe. Siriel Shaidi Mchembe (kushoto) akiwa pamoja na Meneja
wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Bw. David Mahiba pamoja na
Kamati ya Ulinzi na Usalama wakati wakitoa elimu kwa wananchi
walioshiriki zoezi hilo kwa asilimia 100 kwa amani na upendo.
Wananchi wakifuatilia mkutano huo.
Vibanda vya wavamizi wa Hifadhi ya Misitu Gairo vikiteketezwa kwa moto.
Miti
ya asili yenye zaidi ya miaka 35 ikiteketezwa kwa ajili ya kutengeneza
mkaa. Sehemu kubwa ya miti hii ni miti ya mbao ngumu aina ya mitondoro.
Wadau
wa mazingira nchini Tanzania wameombwa kujitokeza kuinusuru wilaya ya
Gairo ambayo inahekari zaidi ya 3,000 zilizokuwa zimevamiwa waharibifu
wa mazingira.
Kauli
hiyo imekuja hivi karibuni baada ya Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel
Shaidi Mchembe kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama
kutekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa lakuwaondoa
wavamizi wa Misitu ya Hifadhi kabla ya Disemba 31, 2017.
Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo alipokuwa akiahitisha Bunge la mjini Dodoma Novemba 18, 2017. Kati ya maeneo ambayo yalikuwa na uvamizi na uharibifu mkubwa wa mazingira ni Misitu ya Hifadhi Wilaya ya Gairo.
Mkuu
wa Wilaya ya Gairo, Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akiambatana na Kamati ya
Ulinzi na Usalama Wilaya walifanya vikao na wananchi huku wakipitia
muhtasari ya vikao vya nyuma vya ushirikishwaji kuanzia ngazi ya Kijiji,
Kata, Wilaya hadi Mkoa vya kuwaondoa wavamizi hao.
Aidha
kupitia taarifa ya mpango wa matumizi bora ya ardhi ya kijiji hicho
ambayo ilisomwa na mwenyekiti wa Kijiji ikibainisha utengwaji wa maeneo
mbalimbali zikiwemo ekari 1,000 za hifadhi walizogawiwa wananchi kwa
ajili ya kilimo.
Vikao
vilifanyika kuanzia mwaka 2012 wakati huo Mkuu wa Mkoa akiwa Mhe. Kanali
Machibya. Baadae Mkuu wa Mkoa alikuwa marehemu Joel Bendera ambapo
nyumba kadhaa ziliteketezwa.Licha ya juhudi zote hizo bado wavamizi hao waligoma kutoka.
Hivyo
basi, kwa kauli ya Waziri Mkuu zoezi limefanikiwa wavamizi wote
wameondoka katika Misitu Hifadhi ya No. 30 Kijiji cha Kumbulu Kata ya
Chanjale na nyumba zote ziliteketezwa kwa moto.Eneo
hilo la misitu lina ukubwa wa ekari 3,000 limepakana na Wilaya ya
Kongwa na Mpwapwa na kutokana na uharibifu huo mkubwa umesababisha hali
kubwa ya ujangwa kwa Gairo na maeneo ya Dodoma.
Ikumbukwe
kuwa Wilaya ya Gairo inategemeana sana na Mkoa wa Dodoma kwenye hali ya
hewa kwani uwanda wa juu wa Gairo kupitia milima iliyopo Tarafa ya
Nongwe ni kichocheo kikubwa cha hali ya hewa nzuri makao makuu ya nchi
Dodoma. Ipo misitu mingine kama misitu ya Hifadhi ya Ukaguru ambayo ni
namba tano kwa ukubwa nchini Tanzania. Ipo misitu mingine mikubwa
mitatu.
Zoezi
hilo liliweza kukamilika kwa asilimia 100 lkinachofuata ni operesheni
kubwa ya kupanda miti inayofanywa Wilayani kwa usimamizi makini wa
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia Meneja wake, Bw. David
Mahiba.