Na Mwandishi Wetu.
WASHINDI
20 wa promosheni ya Mlimani City Shoping Fest wamepatika mara baada ya
kucheza droo iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mlimani City jijini Dar es
Salaam ambao ni Grace Mushi,Samson K. Samson,Grace Hoka, Mnyamani, Mushi
Kimaro, Judith Shayo, Erick Msumati, Gwamaka Hezron, Ally Nyaga, Amani
Sepetu, Masood Wanani, Jonathan Nkya, Hellen Mngutu, Omary Khary, Linda
Bahati, Agrum Maringo, Saidi Kheri, Paul Charles, Beatrice Kaswaga na
Suzan Said.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mratibu wa Kampeni hiyo, Neema Utouh alisema
mpaka sasa jumla ya washindi 40 wamepatikana tangu Kampeni hiyo
izinduliwe rasmi na tayari zawadi zao za vocha ya kufanya manunuzi yenye
thamani ya Shilingi 100,000 kila mmoja wameshapatiwa.
Alisema
Neema, ni nafasi yakow ewe ambaye hujaja kufanya manunuzi mlimani City
karibia fanya manunuzi ya shilingi laki moja au zaidi utapewa kuponi
ambayo itakuwezesha kuingia moja kwa moja kwenye droo ya ushindani.
Hii
ni wiki ya pili taku promosheni hii izinduliwe na bado wiki tatu ambapo
mwisho kabisa kutakuwa na droo kubwa ambayo mshindi mmoja atajishindia
vocha yenye thamani ya shilingi 10,000 000 ambayo itamuwezesha kufanya
manunuzi duka lolote ndani ya Mlimani City pamoja na washindi watano
watakaojishindia vocha yenye thamani ya shilingi milioni moja kila
mmoja.
Mwisho
Neema alitoa wito kwa wateja wa mlimani City na watu wote kujitokeza
kwa wingi kuja kufanya manunuzi Mlimani City katika kipindi hiki cha
siku kuu ya Chrismass na Mwaka mpya ili kupata fursa ya kushiriki katika
shindano la promosheni ya “Mlimani City Shopping Fest”.
AKatika
kusherehekea Sikukuu za X-Mas na Mwaka Mpya, uongozi wa Mlimani City
kwa kushirikiana na wafanyabiashara wenye maduka ndani yake umetangaza
ofa maalumu kwa wateja wake watakaofanya manunuzi katika msimu huu wa
sikukuu.
Ofa
hiyo inatoa fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali ambazo zimegawanywa
kwa makundi matano ambapo kila wiki washindi 20 watajishindia vocha
yenye thamani ya kufanya shoping kwa vitu vya thamani ya Shilingi
100,000 lakini pia watakuwa mwameingia moja kwa moja kwenye droo kubwa
ya mwisho ambayo mshindi wa kwanza atajishindia vocha ya manunuzi ya
bidhaa za nyumbani yenye thamani ya Shilingi Milioni 10, na mshindi 5
watajinyakulia vocha yenye thamani ya shilingi milioni 1, kila mmoja.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja mkuu wa Mlimani
City Ndugu Pastory Mrosso alisema kuwa washindi wa kila wiki watafanya
manunuzi katika duka lolote ndani ya Mlimani City kwa kutumia vocha zao.
Promosheni
hii maalumu imeanza Desemba 15 na inatarajia kufikia mwisho Januari 14,
2018, ambapo droo kubwa ya kupata mshindi wa kwanza wa Vocha yenye
thamani ya Shilingi milioni 10.
Meneja
huyo aliwaomba watanzania kuendelea kufanya manunuzi yao katika maduka
ya Mlimani City, kutokana na kuwajali wateja wake na kutoa huduma
zinazokwenda na wakati na hasa katika kipindi hiki cha X-Mas na Mwaka
Mpya.
Coordinator/Mratibu
wa promosheni ya fanya manunuzi mlimani City na ushinde(Grand Shopping
fest), Neema Utouh akichanganya kuponi ili kupata washindi 20 wa droo ya
pili wa vocha ya thamani ya Shilingi 100,000 kila mmoja ya kufanya
manunuzi tena katika duka lolote ndani ya Mlimani City iliyofanyika
mwishoni mwa wiki Mlimani City Dar es Salaam.Wengine ni mabalozi wa
Promosheni hiyo.
Coordinator/Mratibu
wa promosheni ya fanya manunuzi mlimani City na ushinde(Grand Shopping
fest), Neema Utouh akifungua kuponi ya msindi wa kwanza wa droo ya pili
wa vocha ya thamani ya Shilingi 100,000 ya kufanya manunuzi tena katika
duka lolote ndani ya Mlimani City iliyofanyika mwishoni mwa wiki Mlimani
City Dar es Salaam.Wengine ni mabalozi wa Promosheni hiyo.
Coordinator/Mratibu
wa promosheni ya fanya manunuzi mlimani City na ushinde(Grand Shopping
fest), Neema Utouh(kushoto) akimkabidhi vocha ya thamani ya Shilingi
100,000, Grace Mushi mara baada ya kuibuka mshindi katika droo ya pili
ya promosheni ya fanya manunuzi Mlimani City na ushinde(Mlimani City
Grand Shopping Fest) iliyofanyika Mlimani City mwishoni mwa wiki.