Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Ligi
Kuu ya Wanawake Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Novemba 26, 2017
katika vituo viwili vya Dar es Salaam na Arusha, imefahamika.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Salum Madadi amesema Kundi A litakuwa Dar es Salaam na timu za Simba
Queens ya jijini Dar Es Salaam iliyopanda daraja msimu huu.
Timu nyingine kwenye kundi hilo ni Mburahati Queens, JKT Queens,
Evergreen zote za Dar es Salaam pamoja na timu za Fair Play ya Tanga na
mabingwa watetezi – Mlandizi Queens.
Kundi B litakuwa na timu za Alliance ya Mwanza ambayo imepanda kutoka
kituo cha Dodoma. Timu nyingine ni Marsh Academy pia ya Mwanza; Panama
ya Iringa; Kigoma Sisterz ya Kigoma, Baobab ya Dodoma na Majengo Queens
ya Singida.
Time hizo zitapambana katika vituo hadi Desemba 9, mwaka huu kabla ya
kutoa jumla ya timu nane kwa maana ya nne kutoka kila kundi. Timu hizo
nane zitapambana katika hatua ya Nane Bora ya Ligi hiyo kuelekea
ubingwa. Ligi inatarajiwa kumalizika Machi 28, mwakani.
Kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, TFF imetoa kalenda ya mashindano hayo
ambako usajili utakuwa kati ya Oktoba 25 na Novemba 10, mwaka huu.
Novemba 12 hadi 17, mwaka huu ni kipindi cha pingamizi wakati
Novemba 18, mwaka huu kutakuwa na kikao cha Kamati ya Sheria kabla ya
Novemba 20, mwaka huu kutoa leseni za wachezaji.
Novemba 24, mwaka huu kutakuwa na Semina ya Viongozi wa klabu, Waamuzi na Makamishna jijini Dar es Salaam.
Baada ya kumalizika hatua ya makundi Desemba 9, mwaka huu Ligi Kuu hatua ya Nane Bora ‘Super 8’ itaanza Desemba 20, mwaka huu.
EmoticonEmoticon