Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Kocha
Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Sweden,Mariane Sundhage leo Oktoba
23, 2017 amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Stephen Kebwe
katika Ofisi ya Mkoa na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuboresha soka
la wanawake nchini.
Kadhalika, Kocha Mariane Sundhage amefanya mazungumzo yanayofanana na
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Wallace Karia ambaye
baadaye aliongozana naye kwenda kuangalia Kliniki kwenye Chuo cha
Maendeleo ya Wananchi Bigwa.
Katika Kliniki hiyo, mbali ya Rais Karia wengine waliokuwako
kushuhudia kliniki hiyo ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake
(TWFA), Amina Karuma na Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya soka la
Wanawake, Mia Mjengwa.
Kocha Mariane Sundhage yuko nchini Tanzania na kesho Jumanne Oktoba
24, 2017 anatarajiwa kuwa na kliniki maalumu kwenye Uwanja wa Karume,
Ilala jijini Dar es Salaam.
Kocha huyo mahiri ambaye mbali ya Sweden ambako anafundisha sasa, tayari alikwisha kuzinoa timu za taifa za Marekani na China.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Salum Madadi, kliniki hiyo itaanza saa 3.30 asubuhi
mpaka saa 6.00 mchana baada ya hapo kocha huyo atakuwa na nafasi ya
kuzungumza na wanahabari.
“Karibu sana wanahabari kesho kushuhudia ufundi wa Kocha Pia Sundhage
akizinoa baadhi ya timu ambazo TFF imezialika wakiwamo wachezaji wa
timu ya taifa,” amesema Madadi alipokuwa anatambulisha ziara ya kocha
huyo.
EmoticonEmoticon