Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Genesta Mhagama akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jaffo wakati wa uzinduzi wa namba maalum ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti ukimwi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Genesta Mhagama akimkabidhi Hundi ya Tsh. Mil 200 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mererani wakati wa uzinduzi wa namba maalum ya kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jaffo akikabidhi hundi ya Tsh mil 200 kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Mererani; Fedha hizo ni kutoka kwenye Mfuko wa udhamini wa kudhibiti ukimwi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jaffo(aliyesimama) akitoa neno la Shukrani baada ya kukabdhiwa Tsh Mil 200 za Ujenzi wa Kituo cha Afya Mererani kutoka katika Mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu
Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Genesta
Mhagama(katikati) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jaffo(tatu kulia), Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu(tatu
kushoto) pamoja na viongozi wengine baada ya uzinduzi wa namba maalumu
ya kuchangia mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi.
……..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Genesta Mhagama
amemkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhe. Selamani Jaffo Tsh mil 200,000 kwa ajili ya ukarabati wa
kituo cha Afya Mererani ikiwa ni ahadi ya Rais Dr.John Magufuli
aliyoitoa wakati wa ziara yake Mkoani hapo mwezi uliopita.
Ujenzi wa Kituo hicho ambao utaboresha
huduma za mama na mtoto pia ni maalumu kwa ajili ya kusaidiazaidi
katika kutoa huduma kwa watu walioathirika na virusi vya ukimwi katika
Wilaya ya Simanjiro.
Ikiwa ni miongoni mwa Wilaya
zilizoathirika zaidi na virus vya Ukimwi haswa katika eneo la mererani
imeonekana inahitaji msaada wa haraka ili kudhibiti au kupunguza kabisa
tatizo hilo katika jamii ya eneo hilo.
Fedha hizo zimetoka katika mfuko wa
udhamini wa udhibiti wa Ukimwi ambao ulizinduliwa mwishoni mwa mwaka
jana na kuanza kazi rasmi ya kukusanya fedha kutoka katika vyanzo vya
ndani kusaidia katika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Akipokea Hundi hiyo Waziri wa Tamisemi
Mhe. Selemani Jaffo kabla ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe
Joel Bendera amesema umefika wakati ambapo jamii ya watanzania wanapaswa
kuunga mkono jitihada hizi ili kupunguza maambukizi ya virusi vya
Ukimwi.
Wakati huo huo Tume ya kudhibiti
Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imezindua rasmi namba maalum ya kuchangia
Mfuko huo wa udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.
Katika uzinduzi huo ambapo mgeni Rasmi
alikua Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira
na Walemavu Mhe. Genesta Mhagama alitaja namba ya uchangiaji wa mfuko
huo kuwa 0684909090 na kwamba kila mwananchi anahimizwa kuchangia Fedha
ili fedha itakayopatikana isaidie watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.
Katika hatua Nyingine Waziri Mhagama
alimkabidhi hundi ya Tsh. Milioni 660 kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu kwa ajili ya kununua
dawa aina ya Contrimaxozole za watu wanaoishi na VVU.
Fedha zote hizi zimetoka katika Mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi.
TAMISEMI YA WANANCHI
EmoticonEmoticon