Makocha
28 wanawake kutoka vyuo mbalimbali vya Maendeleo ya Jamii nchini leo
Oktoba 17, 2017 wamehitimu kozi fupi ya ukocha katika kozi iliyoratibiwa
kwa pamoja kati ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na
Taasisi ya Karibu Tanzania (KTO).
Kozi
hiyo ya siku mbili ambayo ni ya pili kufanyika kwa makocha hao,
iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume - Makao Makuu ya TFF ilikuwa chini
ya mkufunzi wa TFF, Raymond Gweba.
Akizungumza
kwenye ufungaji wa kozi hiyo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Yusuph
Singo(Pichani) amesema Serikali inafahamu kuwa inatakiwa kuwekeza kwenye soka la
wanawake kuanzia upande wa vijana na ndio maana inatengeneza mazingira
na sera zitakazowezesha mafanikio hayo.
Singo
amesema nchi mbalimbali wana maendeleo makubwa katika mpira wa miguu
kwa wanawake na sasa wakati wa Tanzania kuwekeza katika upande huo
kuanzia kwa watoto na makocha.
Kadhalika,
Singo amewataka wahitimu kuchukuwa mafunzo hayo kwa uzito mkubwa kwa
sababu mpira wa miguu ya ajira na elimu hiyo itaongeza kitu kikubwa
kwao.
Naye,
Mwenyekiti wa Chama Mpira wa la Wanawake (TWFA), Amina Karuma amesema
lengo la chama chake na TFF kuhakikisha soka linachezwa nchi nzima
linaelekea kutimia.
Amewataka
wahitimu hao wa kozi hiyo fupi kuvitumia vyeti walivyovipata kuendeleza
soka la wanawake na kufanyia kazi yale yote waliyofundishwa.
Pia ameiomba Serikali kuwaunga mkono katika maendeleo ya soka la wanawake.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Salum Madadi amesema
kufundisha watoto kuna changamoto nyingi, lakini makocha hao
wamefundishwa maarifa ya jinsi ya kukabiliana nazo.
Amesema
maarifa hayo sio makocha wote wanaweza kuyapata lakini wameona umuhimu
mkubwa kwa wahitimu hao kuweza kuyapata ili kwenda kuibua vipaji kuanzia
chini.
Wahitimu wa kozi hiyo wamepatiwa vyeti vya ushiriki na vifaa vya michezo ikiwemo koni na mipira.
EmoticonEmoticon