Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akifafanua jambo kwa watumishi
wa ofisi yake (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya wiki ya Utumishi
wa Umma yenye kauli mbiu “Kuimarisha Ushirikishwaji wa Jamii katika
Utoaji Huduma: Vijana washirikishwe kuleta Mabadiliko Barani Afrika”
Waliyoadhimishi Dodoma Juni 22, 2017 kulia aliyekaa ni Katibu Mkuu
(Waziri Mkuu na Bunge) Bi. Maimuna Tarishi.
Baadhi ya watumishi Ofisi ya
Waziri Mkuu wakimsikiliza Katibu Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi
Mwinyimvua (hayupo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika Ukumbi wa
Mikutano ofisi hiyo Dodoma ili kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma
inayoendelea Barani Afrika.
Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimaliwatu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Issa Nchansi akieleza kanuni za
maadili kiutendaji kwa watumishi wa ofisi hiyo wakati wa kuadhimisha
Wiki ya Utumishi wa Umma walipokutana na watumishi wote Dodoma ili
kujadili masuala ya kiutumishi Juni 22, 2017.
Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli za
Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akisoma Kanuni za
Maadili ya Utendaji Katika Utumishi wa Umma wakati wa maadhimisho ya
Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo ofisi hiyo imeadhimisha kwa kukutana na
watumishi wake kujadili masuala ya msingi ya kiutumishi Juni 22, 2017.
Msaidizi wa Waziri Mkuu (Hotuba)
Bw. Abdalah Mtibora akiuliza swali kwa Mwenyekiti wa mkutano (hayupo
pichani) wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika
Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma tarehe 22Juni, 2017.
Mhasibu Ofisi ya Waziri Mkuu
Bi.Kissa Mwakipesile akieleza hoja yake kwa Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimaliwatu ofisi hiyo Bw.Issa Nchansi (hayupo pichani) wakati wa
maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika Juni 22, 2017
Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
Afisa Tehama Ofisi ya Waziri Mkuu
Bw.Innocent Mboya akifafanua jambo kwa washiriki wa mkutano wa
maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika Juni 22, 2017
katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na
Bunge) Bi. Maimuna Tarishi akifunga mkutano wa wafanyakazi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu Dodoma wakati wa kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma
inayoadhimishwa kila mwaka kuanzia tarehe 16-23 Juni Barani Afrika.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)
……………………………………………………………………………
Na. Mwandishi Wetu
Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu
wameaswa kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia maadili na utendaji
katika Utumishi wa Umma wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa
Umma.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu Dkt. Hamisi
Mwinyimvua alipokutana na wafanyakazi wa ofisi yake Dodoma kwa lengo la
kuiadhimisha Wiki hiyo inayofanyika kila mwaka kuanzia Juni 16-23 Barani
Afrika ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kuimarisha Ushirikishwaji wa
Jamii katika Utoaji Huduma: Vijana washirikishwe kuleta Mabadiliko
Barani Afrika”.
“Kila mtumishi wa umma anapaswa
kuwa mwadilifu na mchapakazi hivyo niwaombe watumishi wote muwe mfano
kwa kuwa waadilifu katika utendaji wenu kwa kuzingatia sheria zote za
utumishi wa umma ili kuisaidia Serikali na kuwafikia wananchi
kiujumla.”alieleza Dkt.Mwinyimvua
Katika kuiadhimisha wiki hii ya
utumishi wa Umma ni wakati pekee wa kujitathimini eneo la kiutendaji na
kuona maeneo yenye mapungufu ili yafanyiwe maboresho kwa haraka lengo
likiwa kuondokana na mazoea yaliyokuwepo na kuendana na kasi ya Serikali
ya Awamu ya Tano.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali watu, Issa Nchansi amewataka watumishi kuzingatia
mambo nane muhimu yaliyoainishwa katika Kanuni za Maadili ya Utendaji
katika Utumishi wa Umma ikiwemo; Utoaji wa huduma bora, Utii kwa
Serikali, bidii ya kazi, kutoa huduma bila upendeleo, uwajibikaji kwa
umma,kuheshimu sheria, matumizi sahihi ya taarifa na uadilifu sehemu ya
kazi.
Naye, Katibu Mkuu (Waziri Mkuu na
Bunge) Bi. Maimuna Tarishi aliwaomba watumishi wote kuzingatia kauli
mbiu ya mwaka huu kwa kuwawezesha vijana kielimu, kiuchumi na kijamii
ili waweze kuzalisha na kuwa tegemeo la taifa.
“Niwaombe watumishi wote
kuiangalia hili kundi la vijana wanaoajiriwa na Serikali kwa kuwatia
moyo na kuwaunga mkono katika utekelezaji wa kazi zao” alisisitiza
Tarishi
Sambamba na hili, Katibu Mkuu,
Tarishi alisema kuwa ili kuwe na utendaji wenye matokeo lazima kuitumia
wiki hii kukumbushana majukumu na nafasi zetu katika kuitumikia
serikali.
“Tuwe na utendaji wenye matokeo na si kuhesabu siku, miezi hadi mwaka bali tuwajibike kwa uadilifu kila muda tuwapo Serikalini.”
EmoticonEmoticon