DTB BENKI KUPANUA WIGO WA HUDUMA ZAO MKOANI TANGA

June 22, 2017
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumza wakati wa futari iliyoandaliwa na Benki ya DTB kwa ajili ya wateja wao mkoani Tanga  iliyofanyika kwenye hotel ya Tanga Beach Resort,kulia ni Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu na kushoto ni Meneja wa Benki ya DTB Mkoani Tanga,Athumani Juhudi
 MKUU wa wilaya ya Tanga,Thobias mwilapwa akizungumza wakati wa futari hiyo
 Shehe wa Mkoa wa Tanga,Juma Luwuchu akitoa neno kwenye futari hiyo
 Meneja wa Benki ya Diamond Trust Bank Mkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi akizungumza na waandishi wa habari
 Wageni waalikw
 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Daudi Mayeji kushoto akisalimiana na Aliyekuwa Meya wa Jiji la Tanga,Alhaj Kassim Kisauji wakati wa hafla ya futari hiyo
 sehemu ya wageni waalikwa wakipata futari

BENKI ya Diamond Trust(DTB) Tawi la Tanga wanakusudia kupanua wigo wa huduma zao kwa wateja kwa kukarabati na kuongeza namba ya wahudumu ikiwa ni mkakakti wa ujio wa fursa mbalimbali mkoani hapa ukiwemo mradi mkubwa wa bomba la mafuta kutoka hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.

Hayo yalibainishwa juzi na Meneja wa Benki ya Diamond Trust Bank Mkoani Tanga (DTB) Athumani Juhudi wakati futari iliyoandaliwa na Benki hiyo kwa wateja wao wa mkoa wa Tanga iliyofanyika kwenye ukumbi wa Tanga Beach Resort mjini hapa na kuhu dhuiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya za Handeni na Tanga.

Alisema wao wanakusudia kufanya hivyo ili kuweza kuendana na wigo mpana wa ukuaji wa uchumi kwa mkoa wa Tanga ambao unatarajiwa kufanyika kutokana na mradi huo mkubwa .

“Benki yetu ipo kwenye nafasi ya tano kati ya mabenki zenye amana kubwa za wateja hivyo tumeona kuwaandalia futari hiyo ni namna bora ya kuwashukuru wao kwa kuwasapoti”Alisema.

“Unajua wateja wetu wamekuwa wakitusapoti hivyo ndio maana tumeona vizuri kuwaandalia futari lakini pia niwaambie kuwa  wanaweza kutuma na  kusafirisha fedha kwa haraka kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi”Alisema

Awali akizungumza katika hafla hiyo,Mkuu  wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella aliwataka wakazi wa mkoa huu kuendelea kumuombea Rais John Magufuli aweze kuendelea kupigania haki za watanzania wanyonge ambazo zimekuwa zikipotea.

Alisema kuwa kiongozi huyo mkuu wa nchi amekuwa akifanya mambo makubwa ya kuhakikisha watanzania wanapata maendeleo haraka na kukuza uchumi ambao utatufikisha kwenye mafanikio.

“Ndugu zangu waislamu tuendelee kuombea nchi yetu na Rais wetu ili yeye na viongozi wote waendelee kutenda yaliyomema na yanayompendeza mwenyezi mungu”Alisema RC Shigella.

“Lakini pia niendelee kuwashukuru kwa kuendelea kudumisha amani na mshikamano kwa mkoa huu kwa kipindi cha tokea mwezi ulipoanza mpaka sasa  hivyo muendelee kuwa na upendo kwa watu wote.

Awali akizungumza katika futari hiyo,Shehe wa Mkoa wa Tanga, Juma Luwuchu  aliwataka waislamu mkoano hapa kuendelea mshikamano waliokuwa nao kwenye kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kuendelea kutenda yaliyo mema.

“Tuendelee kushikamana tupendane lakini kubwa zaidi tuhakikisha tunazingati kufanya ibada mara kwa mara na sio kipindi cha mwezi huutu hata baada ya kumalizika kwake “Alisema.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »