Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya
picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini
aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika
hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi
huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini
kwao Ujerumani. Waziri Maghembe alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano
na misaada mbalimbali aliyoitoa, yeye binafsi na nchi yake katika kusaidia kuendeleza sekta ya uhifadhi nchini.
Balozi
wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (katikati)
akifurahia zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori alivyopewa na
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) katika
hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la
Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho
Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi. Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya
picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini
aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika
hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi
huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini
kwao Ujerumani. Kulia
ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence
Milanzi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA, Martin Loibooki.
Balozi
wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kushoto)
akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la
Akiba la Selous mkoani Morogoro.
Balozi
wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kulia)
akimkabidhi Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe zawadi ya picha
ya kumbukumbu ambayo ilipigwa wakati wawili hao wakitua kwa ndege katika
uwanja wa ndege wa Matambwe, Selous, Kwa mujibu wa balozi huyo siku
hiyo haikuwa rahisi kwa ndege hiyo kutua kwa kuwa mvua zilikuwa
zinanyesha. (PICHA NA HAMZA TEMBA – WMU)
EmoticonEmoticon