KATIBU MKUU - UTUMISHI AKUTANA NA WATUMISHI WA MKOA WA SINGIDA NA KUHIMIZA SUALA LA UADILIFU

June 22, 2017
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (wa pili kulia), akifafanua jambo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi (kushoto) baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji ya Mkoa wa Singida kutoka kwa Katibu Tawala huyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
 Baadhi ya Watumishi wa Mkoa wa Singida wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. 
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akiongea na watumishi wa Mkoa wa Singida wakati wa kikao kazi na watumishi hao ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akipokea maoni na malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Singida wakati wa kikao kazi na watumishi hao mkoani Singida ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. Kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dkt. Angelina Lutambi.
 Mmoja wa watumishi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida akitoa maoni wakati wa kikao kazi na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017. 
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akifafanua jambo kwa mmoja wa watumishi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida alipokuwa akisikiliza malalamiko ya mtumishi huyo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.
Afisa TEHAMA Mwandamizi kutoka Ofisi ya Rais - Menejementi ya Utumishi wa Umma, Bi, Jeanfrida Mushumbusi akihakiki taarifa za mmoja wa watumishi kutoka mkoa wa Singida ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2017.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »