Mbio
za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon zimezinduliwa rasmi leo
Jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Chama Cha Riadha Tanzania, wadhamini na waandaaji.
Akizindua
mbio hizo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Mh. Dk.
Harrison Mwakyembe alisema Kilimanjaro Marathon imejizolea umaarufu
mkubwa kwa kuwa maandalizi yake ni mazuri na kuwataka waandaaji wa mbio
nyingine kuiga mfano huu.
“Tunataka
kuwaibua kina Felix Simbu wengine na hili linawezekana tu kupitia mbio
kubwa kama Kilimanjaro Marathon. Nimefahamishwa kuwa Simbu pia alitokana
na mbio hizi kwani aliwahi kushiriki kilometa 21 miaka ya nyuma...sisi
kama serikali tutafanya kila linalowezekana kuyafikia malengo haya,”
alisema.
Alishukuru
pia wadhamini wengine ambao ni Tigo-21km, Grand Malt 5km na wale wa
meza za maji ambao ni pamoja na First National Bank, Kilimanjaro Water,
Diamond Motors Ltd, Kibo Palace, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar,
Simba Cement na KNAUF Gypsum.
Mkurugenzi
wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis alisema wanajivunia kudhamini
mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ambazo zinakuwa kwa
kasi kubwa mwaka hadi mwakana hii inawapa moyo na ari ya kuendelea kuwa
wadhamini.
Alisema
udhamini huu katika mbio za kilometa 42 na 5 kupitia Grand Malt, pamoja
na mambo mengine unalenga kuibua vipaji zaidi katika riadha na kuwataka
washiriki kujiandaa vizuri. “Inabidi tujiamini zaidi kwani siku moja
wimbo wa Taifa wa Tanzania utapigwa katika mbio maarufu duniani,”
alisema.
Meneja
wa Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli alitoa rai kwa washiriki
kuhakikisha wanajiandikisha mapema li kuepuka usumbufu dakika za mwisho
na kutoa mfano wa mwaka huu ambapo namba za ushiriki zilikwisha kutokana
na watu wengi zaidi kujitokeza. “Tumeshazungumza na waandaaji ili
kuwepo na namba za kutosha mwakani,” alisema.
Alisema
ujumbe mkuu wa Kilimanjaro Premium Lager kwa mbio za mwakani ni ‘Kunywa
kistaarabu usiendeshe ukiwa umekunywa’.”Najua wengi tungependa
kufurahia kili zetu baridi baada ya mashindano lakini tunywe kwa
ustaarabu,” alisema huku akiongeza kuwa zawadi kwa mshindi wa kilometa
42 ni milioni 4 kwa mwanaume na mwanamke na jumla ya zawadi ni milioni
20 kwa washindi wote.
- Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis akizungumza kuhusu udhamini wa mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 zitakazofanyika mwakani Machi 4 mkoani Kilimanjaro. Kushoto Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli na Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe.
Kaimu
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini,,Henry Kinabo alisema, “Tuna
furaha kuwa sehemu ya mbio hizi kwa mara nyingine. Hizi ni mbio ambazo
zinawaleta pamoja wanariadha wakubwa na watu kutoka Nyanja mbalimbali
kusherekea michezo, kufurahi, kukuza utamaduni, utalii na pia kwa afya
bora,” alisema.
Alisema
Tigo, inayodhamini mbio za kilometa 21, itatoa jumla ya Milioni 11 kama
zawadi huku msindi wa kwanza wa kiume na kike wakijinyakulia milioni 2
kila mmoja wa pili milioni 1 wakati wa tatu watapokwa Tsh 650,00o huku
Katia ya 500,000 na 100,000 zikienda kwa washindi kuanzai wan ne hadi wa
10 pamoja za medali za ushiriki kwa kila atakayemaliza mbio.
Meneja
Masoko wa TBL anayesimamia kinywaji cha Grand Malt, Warda Kimaro,
alisema mbio za Kilometa 5 zinazodhaminiwa na Grand Malt zinakuwa mwaka
hadi mwaka na kuwavutia watu wengi zaidi wakiwemo watoto, vijana na watu
wazima. “Tumeandaa shughuli mbalimbali za kusisimua kwa ajili ya
washiriki kwa hivyo tujiandikishe mapema na tukumbuke kunywa Grand malt
kwa kuwa ni kinywaji chenye afya hasa kwa wanariadha,” alisema.
Kilimanjaro
Premium Lager Marathon huandaliwa na Wild Frontiers na Deep Blue Media
na kuratibiwa na Executive Solutions. Wadau wengine muhimu ni, Chama Cha
Riadha Tanzania, Chama Cha Riadha Mkoa wa Kilimanjaro, Kilimanjaro
Marathon Club, Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,vilabu vya jogging na Jeshi
la Polisi.
- Makamu wa Rais wa Chama Cha Riadha Tanzania, William Kallaghe akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio za 16 za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 zitazofanyika machi 4 mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe. na Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis.
- Pichani juu na chini ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Dk Harrison Mwakyembe (katikati) akizindua rasmi mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2018 leo Jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa TBL Group anayesimamia Grand Malt, Warda Kimaro, Kaimu Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini Henry Kinabo, Katibu Mkuu wa TOC Filbert Bayi, Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo, Alex Nkenyenge, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager Pamela Kikuli, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Thomas Kamphuis na Makamu wa Rais wa Chama Cha Riadha Tanzania, William Kallaghe.