SERIKALI YASHAURIWA KUWEKEZA NGUVU KWENYE TASNIA YA FILAMU

October 25, 2017


 MSANII wa filamu nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Paparazi Intertaiment,Simon Mwapagata maarufu Rado akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga kuhusu uzinduzi wa filamu yake mpya ya “Bei kali” ambayo itakuwa ya kihistoria kwa kuizindua katika ukumbi wa Majestic Sinema siku ya Jumamosi oct 28 mwaka huu kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanga (TD FAA),Mohamed Majuto na kulia ni Katibu wa Chama hicho,Raphael Kiango
 MSANII wa filamu nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Paparazi Intertaiment,Simon Mwapagata maarufu Rado akiwaonyeshawaandishi wa habari mkoani Tanga kava la filamu yake mpya ya “Bei kali” ambayo itakuwa ya kihistoria kwa kuizindua katika ukumbi wa Majestic Sinema siku ya Jumamosi oct 28 mwaka huu kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanga (TD FAA),Mohamed Majuto na kulia ni Katibu wa Chama hicho,Raphael Kiango
 Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Nyumbani iliyopo Jijini Tanga
SERIKALI ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli imeshauriwa kuwekeza nguvu kwenye tasnia ya filamu za kitanzania ambazo zinaweza kusaidia vijana kuweza kujikwamua kiuchumia kwa kutoa ajira kama itakavyokuwa kwenye viwanda.
Ushauri huo ulitolewa na Msanii muigizaji wa tasnia ya Filamu hapa nchini maarufu kama (Bongo Muvi) Saimon Mwapagata “Rado”ambapo alisema kutokana na uwepo wa soko kubwa la filamu linaweza kusaidia kuajiri vijana wengi wa kitanzania.

Alisema iwapo tasnia hiyo ikitiliwa mkazo na kuwepo kwa usimamizi makini ambao utaweza kusaidia wasanii kuweza kupata mafanikio kitendo ambacho kitawawezesha kulipa kodi na kuinua uchumi wa nchini.

Sanjari na hayo lakini msanii huyo ambaye yupo jijini Tanga alisema atazinduzi wa filamu yake mpya ya “Bei kali” ambayo itakuwa ya kihistoria kwa kuizindua katika ukumbi wa Majestic Sinema siku ya Juma mosi oct 28 mwaka huu.

Alisema uwepo wa tasnia hiyo ni sawa na kiwanda kisichokuwa na hasara iwapo watawekewa mazingira mazuri ikiwemo kudhibiti matapeli wanaoihujumu tasnia hiyo hali inayosababisha waandaaji wa filamu hizo kukosa haki zao za msingi za mauzo na kuisababishia serikali kukosa mapato kupitia tasnia hiyo.

“Tunamuona Rais wetu anavyohangaika na uchumi wa viwanda lakini amesahau kuwa tasnia ya filamu ni viwanda visivyokuwa na hasara na ikiwa atahakikishia haki zetu za msingi na kudhibiti walaghai ninaimani Serikali inaweza kuvuna mapato mengi kupitia filamu na kutengeneza ajira nyingi”Alisema.

Aidha alisema filamu hiyo alikwisha ionyesha Mlimani City lakini kutokana na ubora wake na maombi ya watu wengi ameamua kuonyesha Jijini hapa ambapo anatarajia Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigella kuwa Mgeni rasmi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »