Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SHIRIKA
la Viwango Nchini (TBS) limewatangaza washindi wa shindano la uandikaji
wa insha lililoandaliwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP)
lililoshirikisha shule za msingi na sekondari Tanzania nzima.
Akizungumza
kabla ya utoaji tuzo hizo,Kaimu mkurugenzi mkuu wa TBS Egid Mubofu
amesema hatua hii itasaidia sana kuweza kutoa elimu kwa wananchi hasa
baada ya wanafunzi hawa kuonesha jitihada kubwa za kuondokana na suala
zima la uchafuzi wa mazingira.
Katika
shindano hilo lililoshirikisha takribani wanafunzi 75 kutoka sehemu
mbalimbali nchini lilianza rasmi mwezi Septemba na kumalizika mwishoni
mwa mwezi Oktoba na kufanikiwa kupatikana kwa washiriki nane kwa shule
za Msingi na 10 kutoka shule za Sekondari.
Mshindi
wa kwanza kwa upande wa shule ya msingi ilichukuliwa na Nairath Ngururu
kutoka shule ya Wasichana Almutanzir huku nafasi ya pili ikiendelea
Eldred Medard kutoka shule ya Valentine na nafasi ya tatu kwenda kwa
Shiluni Laizer kutoka shule ya Havard zote za Jijini Dar es salaam.
kwa upande wa sekondari,wasichana waliendelea kutamba baada ya
Zainab Kambi kutoka Academic Internaational kushika nafasi ya kwanza,
Frank Kapinga kutoka Kibaha Sekondari kushika nafasi ya pili na nafasi
ya tau kuchukuliwa na Pius Mollel kutoka St Jude
ya Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa mradi huo, Mary Meela amesema kuwa washiriki wote ni
washindi kwani waliweza kuingia kwenye hatua ya mwisho ya mchujo na
wanatakiwa kuja kuwa mabalozi wakubwa katika suala zima la mazingira.
Afisa mwakilishi wa UNEP, Clara Nakenya amesema kuwa hatua hii ni
moja ya malengo 12 yaliyofikiwa kwa ajili ya kupambana na masuala ya
mazingira kwani insha hizi zina elimu ya kutosha kwa rika zote husuani
watoto, vijana na wazee katika kufanya maamuzi kuhusiana na mazingira.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa TBS Egid Mubofu akiwa katika picha ya
pamoja na washiriki wa shindano hilo walioingia fainali pamoja na majaji
wa shindano hilo.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Nchini (TBS) Egid
Mubofu akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano
uandishi wa insha wa mazingira lililoratibiwa na Shirika la Mazingira
Duniani (UNEP) kushirikiana na shirika hilo.
Afisa mwakilishi wa Shirika la Mazingira Duniani (UNEP), Clara
Nakenya akizungumza wakati wa utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano
uandishi wa insha wa mazingira lililoratibiwa na Shirika la Mazingira
Duniani (UNEP) kushirikiana na shirika hilo.
Jaji mkuu wa shindano hilo, Jumanne Mpinga akitolea ufafanuzi
namna washiriki walivyoonyesha juhudi kubwa kwa kuandika insha nzuri
zenye kuleta elimu kwa jamii kuhusiana na mazingira.
Mshindi wa kwanza kwa upande wa shule ya Msingi Nairath Ngururu
kutoka shule ya Wasichana Almutanzir(kushoto) na Mshindi wa kwanza
upande wa shule ya sekondari Zainab Kambi kutoka Academic Internationa
wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu mkurugenzi wa Shirika la Vwiango
Nchini (TBS) Egid Mubofu pamoja na Afisa mwakilishi wa Shirika la
Mazingira Duniani (UNEP), Clara Nakenya.
Mwenyekiti wa mradi , Mary Meela akizungumza wakati wa utoaji wa
zawadi kwa washindi wa shindano uandishi wa insha wa mazingira
lililoratibiwa na Shirika la Mazingira Duniani (UNEP) kushirikiana na
shirika la Viwango Nchini TBS.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Nchini (TBS) Egid
Mubofu akimkabdhi cheti cha heshima kwa jaji mkuu wa shindano hilo
wakati wa iutoaji zawadi kwa washindi na washiriki wengine.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango Nchini (TBS) Egid
Mubofu akikabidhi vyeti kwa washiriki mbalimbali wa Shindano la uandishi
wa Insha inayihusiana na mazingira iliyoratibiwa na Shirika la
Mazingira Duniani (UNEP) kushirikiana na shirika LA viwango nchini TBS.
EmoticonEmoticon