Umoja
wa Ulaya (EU) umewekeza zaidi ya Euro milioni 1 na laki 7 katika kituo
cha Utamaduni cha Makumira kitengo kilichoko ndani ya Chuo Kikuu cha
Makumira ambapo chuo kikubwa cha sanaa kinajengwa pamoja na kumbi ya
burudani itakayogharimu kiasi hicho.
Balozi
wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer
amefanya ziara chuoni hapo ambapo amejionea shughuli za ujenzi
zinazoendelea katika chuo hicho na kusema kuwa kupitia chuo hicho cha
utamaduni wa Tanzania na makabila yake utaendelezwa ili kuleta manufaa
kwa vijana na jamii nzima.
Akizungumza
na wanahabari mara baada ya ziara hiyo amesema kuwa wataendelea kuunga
mkono juhudi za kutunza utamaduni kwani vijana wataweza kutengeneza
fursa za ajira kupitia sanaa za utamaduni.
Meneja
mradi huo Randall Stubbs amesema kuwa kwa sasa wanatoa mafunzo ya ngoma
za utamaduni wa makabila ya wamasai, wameru na wachaga ikiwa ni pamoja
na kufanya maonyesho ya utamaduni katika maeneo mbalimbali.
“Ujenzi
utakapokamilika kutakua na ukumbi wa kisasa, jengo maalumu la mafunzo
kwa utamaduni wa bara la Afrika, Asia na Ulaya ili utamaduni uweze kuwa
endelevu na kurithishwa vizazi na vizazi” alisema Randall.
EmoticonEmoticon