Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo akisisitiza Jambo wakati wa Kikao chake na Bodi
na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Sehemu ya Menejimenti ya TPDC
wakifuatilia kikao baina yao na Waziri wa Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Waziri wa Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza
nchini Sarah Cooke (wa pili kushoto) na ujumbe uliofuatana na Balozi
huo.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo (katikati) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini
Sarah Cooken (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake walipomtembelea leo
ofisini kwake Jijijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamishna Msaidizi wa
Nishati anayeshughulikia umeme, Mhandisi Innocent Luoga.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo katika picha ya pamoja na Naibu Balozi wa Marekani
nchini Virginia Blaser mara baada ya kumaliza mazungumzo yao wakati
Naibu Balozi huyo alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo leo amekutana na Bodi na Menejimenti ya Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), katika kikao kilichochadili
maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na shirika hilo ikiwemo
Mradi wa Kusindika Gesi Asilia, (LNG) na Mradi wa Bomba la Kusafirisha
Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka Hoima nchini Uganda hadi
Bandari ya Tanga.
Katika kikao hicho Prof. Muhongo
ameitaka Bodi na Menejimenti hiyo kuongeza kasi katika utekelezaji wa
miradi husika kutokana na manufaa ya miradi hiyo kwa Maendeleo ya
Taifa.
Mbali na Bodi na Menejimenti ya
TPDC, kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Prof. Justin Ntalikwa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, anayeshughulikia Madini, Prof. James Mdoe na baadhi ya
Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Aidha, wakati huo huo, Waziri
Muhongo pia amekutana na Balozi wa Uingereza nchini Sarah Cooke ambapo
wamejadili masuala kadhaa kuhusu sekta ya nishati ikiwemo chanzo cha
Nishati Jadidifu.
Pia, Waziri Muhongo amekutana na
Naibu Balozi wa Marekani nchini Virginia Blaser ambapo wamejadili
masuala kadhaa kuhusu Sekta ya Nishati.
EmoticonEmoticon