Winga Simon Msuva wa Young Africans amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu ya Vodacom.
Msuva alikuwa na washindani wa
karibu wawili katika kinyang’anyiro hicho cha Oktoba ambao wote ni
kutoka Simba. Wachezaji hao ni Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin.
Katika mwezi Oktoba ambao ulikuwa
na raundi sita, Msuva aliisaidia timu yake kupata jumla ya pointi 14
huku akifunga mabao manne, na kutoa pasi tano za mwisho (assist).
Kwa kushinda tuzo ya mchezaji bora
wa mwezi, Msuva ambaye alikuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa
msimu wa 2014/2015 atazawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa
wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya Vodacom Tanzania.
EmoticonEmoticon