Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Kuelekea pambano la mchezo wa
kimataifa wa kirafiki kati ya Timu ya Tanzania (Taifa Stars)
wanaotarajiwa kucheza na timu ya Taifa ya Zimbwabwe Kocha Mkuu wa
Charles Boniface Mkwasa kwa jina la utani Master ametaja kikosi ambacho
kinatarajia kuingia kambini Novemba 7,2016.
Mkwasa ametangaza majina hayo
wakati akizungumza na waandishi wa habari,amesema kuwa wataanza kambi
hiyo kwa ajili ya mchezo wao na Zimbwabwe na wachezaji wote wataungana
na wengine kuanzia Novemba 13 baada ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu
Tanzania kumalizika.
“Mchezo wetu tunatarajia kucheza
ugenini mjini Harare Novemba 13 hivyo tunauchukulia umuhimu mkubwa kwetu
kutokana kuwa kwenye kalenda ya FIFA na sisi tunataka kushinda kutokana
na kushuka vibaya katika ubora wa viwango vya FIFA na kufika mpaka
nafasi ya 147 kitu ambacho ni hatari kwetu”alisema Mkwasa Wachezaji
wanaounda kikosi hicho ni pamoja na Magolikipa:Aish Manura Azam,Said
Kipao JKT Ruvu na Deogratius Munishi
Mabeki:Erasto Nyoni, David
Mwantika wa Azam, Michael Aidan wa JKT Ruvu, Mwinyi Hajji, Vincent
Andrew wa Yanga, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ wa Simba na James
Josephat wa Prisons.
Viungo:Himid Mao wa Azam ,
Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Jonas Mkude na Muzamil Yassin wa Simba , wakati
viungo wa pembeni ni Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, Shizza Kichuya,
Jamal Mnyate wa Simba na Simon Msuva wa Yanga.
Watupia shavu: Ibrahim Hajib wa Simba , John Bocco wa Azam FC,
Elius Maguli timu ya Oman anacheza , Thomas Ulimwengu aliyemaliza
mkataba wake TP Mazembe ya DRC , Omar Mponda wa Ndanda na Mbwana
Samatta wa K.R.C Genk ya Ubelgiji
EmoticonEmoticon