Ibada
ya Mazishi ya aliekuwa Mkuu wa Vipindi na Afisa Mahusiano katika kituo
cha runinga cha Barmedas Tv cha Jijini Mwanza, Mwalimu Charles Sokoro,
imefanyika jana katika Kanisa la AICT Makongoro na kufuatiwa na mazishi
yaliyofanyika katika Makaburi ya Kitangiri.
Mwalimu
Sokoro ambae pia alikuwa mwalimu wa muziki wa Injili na Mwenyekiti wa
Kwaya ya AICT Makongoro, alifariki jumamosi Julai 16,2016 majira ya saa
mbili usiku katika Hospitali ya Rufaa Bugando baada ya kuugua kwa miezi
kadhaa.
Alizaliwa
mwaka julai mosi mwaka 1965 katika Kijiji cha Kahunda Wilaya ya
Sengerema mkoani Mwanza na hadi mauti yanamkuta alikuwa na umri wa 51
ambapo ameacha watoto wanne, alikuwa mgane.
Na BMG
Kwaya ya AICT Makongoro ikiimba katika ibada ya mazishi ya Sokoro
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la AICT Makongoro akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya mazishi ya marehemu Sokoro.
Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la AICT Makongoro, akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya mazishi ya marehemu Sokoro.
Mmoja wawanafamilia wa marehemu Sokoro akisoma wasifu wa marehemu Sokoro.
EmoticonEmoticon