WACHEZAJI WATATU MISUNA FC WAFUNGIWA

July 20, 2016
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imewafungia wachezaji watatu, walioshiriki katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL), kituo cha Morogoro 2015/2016.

Kikao cha Kamati ya   TFF kilichokaa Julai 14, 2016 kujadilina kupitia malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa RCL kituo cha Mororgoro, kimebaini kwamba wachezaji Imani T. Mwanga, Fred John Lazaro na Brown Chalamila walifanya udanganyifu wa majina ili kukamilisha zoezi la usajili.


KUHUSU MCHEZAJI IMANI T. MWANGA

Kamati imepitia taarifa za waamuzi na Kamisaa pamoja na uthibitisho uliopatikana imemkuta na tuhuma za udanganyifu wa jina. Alitumia majina mawili tofauti. Imani Vamwanga ligi daraja la kwanza klabu cha Kurugenzi FC na Emmanuel T. Mwanga klabu cha Stand Misuna.

Kwa mujibu wa kanuni za ligi ya mabingwa wa Mikoa, kanuni ya 39 (1) Kamati imekufungia kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miezi 12. Adhabu hii inaanza toka tarehe ya kuandi kwa barua yake.

KUHUSU FRED JOHN LAZARO

Kikao cha Kamati ya Mashindano ya TFF kilichokaa Julai 14, 2016 kujadili na kupitia malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa RCL kituo cha Mororgoro, kimebaini kwamba Fred John Lazaro pamoja na klabu ya Stand Misuna FC walifanya udanganyifu wa majina ili kukamilisha zoezi la usajili.

Kupitia taarifa za waamuzi na Kamisaa pamoja na uthibitisho uliopatikana, imebainika Fred John Lazaro alifanya udanganyifu wa majina hivyo kuchezea klabu mbili tofauti katika msimu mmoja isivyo halali.

Katika klabu ya Stand Misuna FC iliyoshiriki ligi ya mkoa Singida na ligi ya mabingwa wa mikoa kituo cha Morogoro 2015/2016 ulisajiliwa kwa jina la Fred John Lazaro kwa usajili namba 044 ukivaa jezi namba 13, pia katika klabu ya Singida United FC ya Singida iliyoko daraja la pili (SDL) msimu wa 2015/2016 ulisajiliwa kwa jina la Adolf Anthon leseni namba 950725003 ukivaa jezi namba 3, 6 na 8 katika mechi tofauti.

Kwa taarifa hapo juu kamati imebaini kuwa wewe siyo mchezaji halali kuichezea timu ya Stand Misuna FC katika ligi ya mabingwa wa mikoa kwa ni hukucheza ligi ya mkoa Singida, na pia kwa kushirikiana na uongozi wa klabu ya Stand Misuna FC umedanganya majina ili kufanikisha zoezi la usajili kinyume cha kanuni ya 48 kipengere cha (2) na (4).

Hivyo kwa mujibu wa kanuni za ligi ya mabingwa wa Mikoa, kanuniya 31 kipengere cha (11) na kanuni ya 39 kipengere cha (1) wewe Fred John Lazaro jezi namba 13 (mchezaji) unafungiwa kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miezi kumi na mawili (12).

Adhabu hiyo inaanza mara moja baada ya muhusika kupata barua yake.

KUHUSU BROWN CHALAMILA

Kikao cha Kamati ya Mashindano ya TFF kilichokaa Julai 14, 2016 kujadilina kupitia malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya ligi ya mabingwa wa mikoa RCL kituo cha Mororgoro, kimebaini kwamba Brown Chalamila pamoja na klabu ya Stand Misuna FC walifanya udanganyifu wa majina ili kukamilisha zoezi la usajili.

Kupitia taarifa za waamuzi na Kamisaa pamoja na uthibitisho uliopatikana umekutwa na makosa ya udanganyifu wa majina hivyo kuchezea vilabu viwili tofauti katika msimu mmoja isivyo halali.

Katika klabu ya Stand Misuna FC iliyoshiriki ligi ya mkoa Singida na ligi ya mabingwa wa mikoa kituo cha Morogoro 2015/2016 ulisajiliwa na kucheza kwa jina la Costa Bryan Bosco kwa usajili namba 029 ukivaa jezi namba 03, wakati wewe ni mchezaji halali wa klabu ya Kurugenzi FC ya Mafinga-Iringa iliyoko daraja la kwanza (FDL) msimuwa 2015/2016 leseni namba 921004001 ukivaa jezi namba 03.

Kwa taarifa hapo juu kamatii mebaini kuwa wewe siyo mchezaji halali wa timu ya Stand Misuna FC katika ligi ya mabingwa wa mikoa kwani hukucheza ligi ya mkoa Singida, na pia kwa kushirikia na uongozi wa klabu ya Stand Misuna FC ulidanganya majina ili kufanikisha zoezi la usajili kinyume na kanuni ya 48 kipengele cha (2) na (4) ya ligi ya mabingwa wa mikoa.

Hivyo, kwa mujibu wa kanuni za ligi ya mabingwa wa Mikoa, kanuniya 31 kipengele cha (11) na kanuni ya 39 kipengele cha (1) wewe Brown Chalamila unafungi wa kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miezi kumi na mawili (12). Adhabu hiyo inaanza mara moja kuanzia tarehe ya barua yakei.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »