Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Wazara ya Maliasili
na Utalii (hawapo pichani) kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha
LAPF, Kijitonyama jijini Dar es salaam Julai 18, 2016 .
………………………………………………………………………………
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameuagiza
uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kubadilisha mfumo wa uvunaji wa
vitatlu vya miti kwenye mashamba ya Serikali ili kuweka uwazi kwenye
biashara hiyo na kuipatia zaidi Serikali mapato.
Mhe.
Majaliwa alisema hayo jana kwenye Mkutano na Viongozi pamoja na
Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga uliopo Kijitonayama Jijini Dar es
Salaam.
Akizungumzia
mabadiliko hayo, Mhe. Majaliwa alisema kuwa utaratibu uliokuwa
ukitumika hapo awali wa kuuza miti kwenye mashamba ya Serikali kwa njia
ya vibali hauna tija kwakuwa umekuwa ukiikosesha Serikali mapato na
kuwanufaisha wafanyabiashara wachache.
“Utaratibu
wa sasa wa kutumia vibali unatuletea migongano ndani ya Wizara na
kuikosesha Serikali mapato, hivyo ni lazima tuubadilishe” Aliongeza
Majaliwa.
Aliuagiza
Uongozi wa Wizara kufanya marekebisho kwenye utaratibu huo na kuweka
utaratibu wa mnada ili kuweka uwazi zaidi na kuondoa manung’uniko kwenye
biashara hiyo. “vibali visitishwe, mnada uanze kama inavyofanyika
kwenye mitiki” Alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Hivi
karibuni Mhe. Majaliwa alisitisha utoaji wa vibali vya uvunaji wa miti
kwenye mashamba matano yanayomilikiwa na Serikali kutokana na kupokea
malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.
Katika
hatua nyingine, Mhe. Majaliwa aliagiza mabadiliko ya haraka katika
vizuizi vya ukaguzi wa Maliasili ambavyo amesema vimekuwa havina tija na
kuagiza baadhi yake vifutwe kabisa. Miongoni vya vizuizi alivyoagiza
vifutwe ni Kibaha Stendi, Kimanzichana na Mbagala, pia aliagiza
kuimarishwa kwa kituo cha Vikindu, Kibiti na Vigwaza.
Mhe.
Majaliwa aliwaagiza wataalamu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
kushirikiana na Tamisemi kwa ajili ya kuweka mfumo mzuri wa kuhifadhi na
kuvuna mazao ya misitu yaliyopo katika Halmashauri na kutenga Misitu ya
Asili tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo kumekuwepo muingiliano katika
kutekeleza majukumu hayo jambo linalopelekea uharibifu wa misitu.
Hapo
awali Mhe. Majaliwa alieleza lengo kuu la Mkutano huo kuwa ni katika
utaratibu wake wa kawaida aliojiwekea wa kutembelea Wizara na kuzungumza
na watumishi kwa ajili kukumbushana majukumu yao, kuangalia changamoto
mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi. Aliwaasa watumishi wa Wizara ya
Maliasili kuwa wazalendo, waadilifu, waaminifu na kuongeza uwajibikaji
ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake ya kuwahudumia vizuri
wananchi.
“Ninyi
ni watu muhimu sana katika utoaji wa huduma kwa wananchi, tekelezeni
majukumu yenu kwa uadilifu wa hali ya juu. Kamilisheni malengo yenu
kulingana na mpangokazi wenu mliojiwekea” Alisema Mhe. Majaliwa.
Kwa
upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe
alisisitiza watumishi wa Wizara hiyo kuhakikisha kuwa wanalinda misitu
kule iliko na sio kusubiri katika vituo na kukamata rasilimali zake
ambazo zimevunwa isivyo halali na kuzitoza faini, kinyume chake
rasilimali hizo zilipiwe kihalali kabla ya kuvunwa. Aliahidi pia kuisuka
upya Idara ya Misitu.
EmoticonEmoticon