MALINZI AWAPA SOMO MAKOCHA

July 20, 2016
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amewataka makocha 20 wanaoshiriki kozi ya ukocha wa leseni A, kwenda kutumia elimu hiyo kusaidia na kuendeleza soka katika nyanja mbalimbali.

Malinzi aliyasema hayo jana Julai 19, 2016 wakati akifungua kozi hiyo ambayo inashirikisha makocha 20 na kufanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.


“Ndugu zangu makocha nawasihi mnapohitimu kozi hii msiende kuweka vyeti vyenu ndani bali mkawe chachu ya mafanikio ya soka kwani kwa idadi ya makocha 23 ambao wana leseni A ni makocha saba tu ambao wanafundisha,” alisema Malinzi.

Pia Malinzi alisema ikimaliza kozi hii Tanzania itakuwa na makocha 43 wenye leseni A jambo ambalo ni idadi ndogo ikilinganishwa na Tanzania ambayo ina watanzania milioni 50.
Pia Malinzi alisema kuanzia msimu huu mpya wa ligi makocha watakaoruhusiwa kuwa na timu za ligi kuu ni wale wenye leseni A na kwa daraja la kwanza ni wenye leseni B huku akisema wasaidizi watatakiwa kuwa na leseni C.

Kozi hii itakuwa inafendeshwa na mkufunzi Sunday Kayuni akisaidia na Salum Madadi na itakuwa ya mwezi mmoja lakini ikimalizika wiki mbili itasimama na kuja kumalizika baadaye.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »