Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
na Misitu wa Serikali ya Czech Republic Bw. Dusan Benza akizungumza
katika kongamano la wafanyabiashara wa nchi hiyo na watanzania
lililofanyika leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
Mawaziri wawili Kilimo na
Viwanda wa Jamhuri ya Jamhuri ya Czech wakiongozana na wafanyabiashara
zaidi ya thelathini wako nchini kwa ajili ya kutafuta na kujionea fursa
za uwekezaji nchini Tanzaniam Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na
Tanzania Investiment Bank (TIB), Ubalozi wa Szech Republic nchini Kenya
na Tanzania House Of Business Company Limited (THB).
Ujumbe huo metembelea wizara ya
Kilimo na wizara ya Viwanda na Biashara na kusaini mikataba ya
ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji hapa nchini na nchi ya Szech
Republic ili kuunganisha masuala ya kibiasha na uwekezaji na kuwezesha
wafanyabiashara wa nchi hizi kuwekeza katika masuala ya biashara,
Teknolojia na Kilimo kwa ujumla.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR
ES SALAAM)
Balozi wa Heshima na Mwakilishi
wa Ubalozi wa Czech Republic hapa nchini John Chaggama akizungumza na
mmoja wa viongozi wa ujumbe huo huku Marian Jureck Waziri wa Kilimo wa
Czech akisikiliz kwa makini.
Injinia Michal Basovnik wa
kampuni ya Impuls akitoa mada kuhusu shughuli mbalimbali zinazotolewa
na kampuni yao ambayo ina tawi pia nchini Zambia.
Injinia Martin Adamuska wa
kampuni ya NWT kutoka nchini Czech Republic akifafanua jambo wakati
alipokuwa akielezea mambo mbalimbali yanayofanya na kampuni yao lakini
pia fursa mbalimbali zinazoweza kuwekezwa.
Injinia Petr Pawlica wa wa
kampuni ya PAWLICA pia ametoa mada katika kongamano hilo na kuelezea
teknolojia ya kampuni hiyo katika masuala ya Kilimo.
Bw. Godffrey Kirenga wa SAGCOT
CENTER LIMITED akiwaelezea wafanya biashara hao juu ya fursa mbalimbali
zilizopo hapa nchini katika uwekezaji wa kilimo.
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa
Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza
katika kongamano hilo kulia ni John Chaggama Balozi wa Heshima na
Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania.
Kutoka kulia ni Mr Charles
Chandika Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania House Of Business
Company Limited, Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech
Consolate nchini Tanzania, Elipina Makungu na Bahija Salim
wakijadiliana jambo wakati wa kongamano hilo la wafanya biashara.
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa
Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza
na Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate nchini
Tanzania wakimsikiliza mmoja wa maofisa kutoka wizara ya mambo ya nje
wakati akizungumza nao.
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa
Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye na John
Chaggama Balozi wa Heshima na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic
nchini Tanzania wakizungumza na Injinia Vladmir Pikora wa benki ya
Czech Export Bank mara baada ya nusu ya kwanza ya majadiliano kati ya
wafanya biashara wa Tanzania na Szech Republic katika kongamano
lililofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.
John Chaggama Balozi wa Heshima
na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ujio wa wafanyabiashara hao.
Mkurugenzi mtendaji Mkuu wa
Tanzania Private Sector Foundation(TPSF) Godfrey Simbeye akizungumza na
waandishi wa habari juu ya umuhimu wa ujio wa wafanyabiashara hao na
kongamano hilo kwa wafanyabiashara wa Tanzania ya Czech Republic katika
masuala mazima ya kibiashara na uwekezaji.
Baadhi ya wafanyabiashara kutoka
nchini Czech Republic wakiwa katika kongamano hilo lililofanyika kwenye
hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam
Baadhi ya wafanyabiashara wa Tanzania wakihudhuria kongamano hilo.
Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali za Tanzania masuala ya biashara na uwekezaji wakiwa katika kongamano hilo.
John Chaggama Balozi wa Heshima
na Mwakilishi wa Ubalozi wa Czech Republic nchini Tanzania
akimsikiliza Pan Arnold Mturi Charge de Affairs at the Szech Consolate
nchini Tanzania.
Elipina Makungu na Bahija Salim
wakifurahia jambo wakati wa kongamano hilo la wafanyabiashara wa Czech
Republic na Tanzania kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.