Fao jipya la Wote Scheme
ambalo ni mfumo wa hiari kwa wanachama ulioanzishwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF
utasaidia kuwapa fursa watanzania waliopo kwenye sekta isiyo rasmi kukidhi
mahitaji na kutambua mchango na ushiriki wa sekta hizo katika kukuza uchumi.
Fao hilo pia linatoa fursa kwa
wafanyakazi waliopo kwenye sekta iliyo rasmi kuwawezesha kunufaika na mfumo huo
kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.
Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa alisema hayo juzi wakati semina kwa askari wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Zimamoto mkoani Tanga uliokuwa na lengo la kuwapa uelewa juu ya mafao yanayopatikana kupitia mfuko huo.
Washiriki wa semina hiyo Meneja wa Mfuko wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa |
Alisema kupitia fao hilo mwanachama
anafaidika na huduma za Afya ikiwemo kupata kadi ya Afya mahali popote kwa
kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini (NHIF) mwaka mzima bure.
Aidha alisema kupitia skimu hiyo mpya ya mfuko huo unachangia na kuwapa uelewa watanzania utamaduni wa kujiwekea akiba ya baadae ili kuweza kukabiliana na ugumu wa maisha wakati wanapokuwa wakifikia umri wa kustaafu.
“Lakini pia sisi kama PPF tunarahisisha uchangiaji kupitia mitandao yote ya simu kwani hii imesaidia kuweza kuepusha changamoto mbalimbali ambazo wanaweza wakukumbana nazo wanachama wetu ambao wamejiunga ma Mfuko huu “Alisema.
Hata hivyo alisema kuwa wanaendelea kutoa mikopo ya elimu na biashara ili kuweza kuwainua wanachama wao kiuchumi sambamba na kujiendeleza kielimu ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha na utandawazi.
“Fao hili lilianzishwa mwezi wa saba mwaka jana ambapo mwanachama
anafaidika na huduma za afya (Kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini - NHIF),mikopo mbalimbali
na Fao la Uzeeni(Pensheni) "Alisema Meneja huyo.
Semina hiyo ililenga kuwapa uelewa wa mambo mbalimbali kuhusu mfuko
huo ikiwemo uandikishaji wanachama,mafao yatolewayo na mfuko huo,Wote Scheme (mfumo
wa Hiari),Mikopo ya Saccos na Fao la Elimu.