Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano, kwa michezo miwili ya viporo
kuchezwa katika viwanja vya Manungu Turiani mkoani Morogoro na uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans wanaoshika nafasi
ya pili kwenye msimamo wa ligi, watakua wenyeji wa Mwadui FC inayokamata
nafasi ya sita katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wakata miwa wa Turiani, Mtibwa
Sugar walio katika nafsi ya nne ya msimamo wa ligi kuu watawakaribisha
Azam FC walio juu yao nafasi ya tatu, mchezo utakaochezwa katika uwanja
wa Manungu Turiani mkoani Morogoro.