Mshiriki
wa mafunzo elekezi juu ya uingizaji wa takwimu za mashauri kwa njia ya
kielectroniki (Judicial Stastical Dashboard System JSDS) kwa Makarani wa
Mahakama Mkoa wa Dar Es Salaam, Bi. Tumaini Mwalioga akisisitiza neno
wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo katika chuo cha LearnIt leo Jijini
Dar Es Salaam.
Mgeni
rasmi Mhe. Solanus Nyimbi (aliyesimama mbele) akitoa nasaha kwa niaba
ya Mtendaji Mkuu Mahakama kwa washiriki wa mafunzo maalum ya uingizaji
wa takwimu za mashauri kwa njia ya kielectroniki kwa Makarani wa
Mahakama Mkoa wa Dar Es Saalaam yanayofanyika katika chuo cha LearnIt
Jijini Dar Es Salaam. Lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha Makarani
waweze kufungua mashauri na kuyaingiza kwa njia ya kiielectroniki. Mpaka
sasa mafunzo hayo tayari yameshatolewa kwa jumla ya Makarani 860. Kwa
upande wa Dar es Salaam mafunzo haya yatatolewa kwa jumla ya Makarani
90.
Kiongozi wa darasa akisoma risala fupi mbele ya mgeni rasmi kabla ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mgeni rasmi katika mafunzo maalum ya mfumo wa kuingiza taarifa ya mashauri (Judicial Stastical Dashboard System (JSDS) Mhe.Solanus Nyimbi (walioketi katikati) Mhe.
Mustapha Sihani, Naibu Msajili Mwandamizi Kanda Kuu Dar es Salaam,
Patricia Ngunguru, Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Mafunzo, Mhe. Said Mkasiwa, Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Ilala, (kushoto) ni kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo