Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikhe Saleh Omar Kabii wakwanza kushoto akitoa maelezo juu ya haki za binaadamu kwa
mujibu wa Uislam wakati alipokuwa akifunguwa Mafunzo ya Haki za
Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa Sheria kwa Viongozi wa Dini,
katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Harusi Miraji na mwisho Jina Mwinyi
Waziri Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma na Sheria.(Picha na Miza
Othman- Maelezo Zanzibar).
Baadhi
ya washiriki wakisikiliza kwa makini maelezo kwa Mufti Mkuu wa Zanzibar
Shekhe Saleh Omar Kabii hayupo pichani katika Mafunzo ya Haki za
Binaadamu na kuwatambulisha wasaidizi wa Sheria kwa Viongozi wa Dini
Mazsons Hotel Zanzibar.
SheikheThabit
Nooman Jongo Afisi ya Mufti Zanzibar akiwafahamisha jambo washiriki wa
mafunzo ya Haki za Binaadamu katika Ukumbi wa Mazsons Hotel Zanzibar.
Picha na Miza Othman-Maelezo Zanzibar).
Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar 01/09/2015.
MASHEKHE
na Walimu wa Madrasa wametakiwa kuwashajihisha wananchi kutojiingiza
katika makundi yanayoweza kuvunja amani kutokana na kufuatiwa kipindi
kigumu cha uchaguzi Mkuu ujao.
Hayo
yameelezwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikhe Saleh Omar Kabii ambae ni
Mgeni rasmini alipokuwa akifunguwa mafunzo ya Haki za Binaadamu
yaliyofanyika katika ukumbi wa Mazsons Hotel ya Shangani Mjini Zanzibar.
Amesema
Masheikhe na Walimu hao ndio wasimamizi wakuu katika maeneo mbalimbali
ikiwemo Miskitini, Madrasani na hata ndani ya Nyumba zao kwani kufanya
hivyo ni kutokiuka sheria iliyopangwa katika Nchi yao.
“
Tofauti za dini, jinsia, cheo na Kabila sio njia za ukiukwaji wa Sheria
ndani ya Nchi yetu bali ni kutii sheria kwani nijukumu la kila
raia,alisema Shekh Saleh Omar Kabii”.
Nae
Shekh Thabit Nooman Jongo kutoka Afisi ya Mufti Zanzibar amewataka
Walimu na Mashekhe wenzake kuwamstari wa mbele katika kusimamia juu ya
ukumbusho huo kwani kufanya hivyo ni kutekelaza majukumu yao.
Aidha
amewataka Masheikhe na Walimu hao kuchukuwa juhudi za hali ya juu na
kutumia maneno ya hekima, busara na unyenyekevu ili waweze kufanikiwa
malengo waliyokusudia.
Hata
hivyo amesema kuwa wakati wanapotoa hutuba zao ndani ya Misikiti na
Madrasa ziwe ni zenye kujenga amani kwani kufanya hivyo ni kuzitii
sheria zilizowekwa katika nchi yao.
Washiriki
wa mafunzo hayo wamesema watayafanyia kazi bila ya kinyongo na
kuyafikisha katika maeneo yao kama walivyoagizwa na Viongozi wenzao.