DOCTER GAO YUN LAI AKIMPIMA PRESHA
NA SUKARI BWANA MOHD ALI MKAAZI WA KISAUNI UPIMAJI HUO ULIFANYIKA
KATIKA KIJIJI CHA KISAUNI ZANZIBAR.
PICHA NA ABDALLA OMAR – MAELEZO ZANZIBAR.
Dokta Fadhil Mohd ambae ni D0kta Dhamana Kanda ya Unguja akitoa maelezo kwa waadishi wa habari (hawapo pichani).
WANANCHI MBALI MBALI WAKIPATAWA HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA KIJIJI CHA KISAUNI ZANZIBAR.
……………………………………………………………….
Mwashungi Tahir Maelezo-Zanzibar
Jumla ya madaktari bingwa tisa
kutoka nchini china wakishirikiyana na madaktari wa hapa Zanzibar
wameweza kutoa huduma za afyakwa wananchi wa shehia ya Kisauni kwa
kuwapima na kuweza kujua afya zao na kuwapatia huduma za matibabu.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi huko katika shehia ya Kisauni wilaya ya Magharibi B Dr
Fadhil Mohammed ambae ni dhamana ya kanda ya Unguja amesema madaktari
hao wamekuja kutoa huduma za afya za jamii hapa Zanzibar.
Amesema madaktari hao wanatoa
huduma hizo vijijini kwa kila baada ya miezi mitatu wanakwenda katika
kijiji chengine kwa lengo la kuwarahisishia huduma hiyo watu hao na
kuwapelekea huduma hiyo katika maeneo yao.
“Lengo ni kuwapelekea wananchi
huduma hiyo karibu na maeneo yao ili waweze kupata urahisi wa kuweza
kujua afya zao” alisema daktari huyo.
Sambamba na hayo Fadhil amesema
jitihada hizi ambazo zinafanywa na madaktari hao na kwa kushirikiana na
Wizara ya Afya ni kuweza kuimarisha huduma hiyo kupitia vijijini ili
kuweza kuwapa muamko wananchi na kuweza kujitokeza kupima afya zao kwa
urahisi.
Madaktari hao bingwa ambao ni
maspeshalisti wa maradhi mbalimbali wameweza kuwapima wananchi maradhi
mbali mbali na kuweza kuwapatia matibabu hapo hapo bila ya usumbufu
wowote.
Maradhi wanayopima na kutoa huduma
ni pamoja na ukimwi, koo, pua, meno, presha magonjwa ya moyo , ganzi,
sukari na matatizo ya mkojo na maradhi mengineyo.
Pia wanatoa huduma za akinamama za
uzazi wa mpango kwa njia salama na huduma za watoto ambapo akinamama
wengi wameweza kujitokeza kwa kujipatia huduma hiyo.
Nae mratibu wa afya wa mama na
mtoto Bi Fatma Ussi Yahya amesema amefurahishwa sana na akinamama wa
kijiji hicho pamoja na majirani kwa kuweza kufika kwa wingi katika
kujipatia na huduma hiyo.
Pia kati ya madaktari hao bingwa
Dr GAO YUNLAI amesema amefarijika sana kuona wananchi wameweza
kujitokeza kwa wingi na kupima vipimo vya aina ya maradhi mbali mbali
ikiwemo maradhi yasiyoambukuza ya kisuari na presha.
Sheha wa shehia hiyo ya Kisauni
Hija Suleiman Othman amewataka wananchi wake wasiidharau huduma hizi
zinapofika vijijini kwani hiyo ni bahati adhimu kwa wananchi wa visiwa
hivi.
“Nimefurahi kuona wananchi wangu
wameweza kuhamasika kwa kujitokeza kwa wingi kwenye huduma hizi ambazo
wameletewa hapa hapa na pia huduma hizi zinatolewa bure kupitia Wizara
ya Afya.” Alisema sheha huyo.
Kwa upande wa wananchi Bi M
wanajuma Omar kutoka mitondooni amesema ameweza kushiriki vizuri katika
kujipatia vipimo na kuweza kujifahamu afya yake ambayo vipimo vyote
alivyoima ameweza kujigundua kuwa yuko salama .
Amewataka akinamama na akinababa
kuweza kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kuweza kujitambua na
kupatiwa matibabu ambapo matibabu hayo yanatolewa kwa wingi hapo hapo
na kuweza kuwaambia kuwa kinga bora kuliko tiba.
Madakatari hao ni maalum Chinese
medical team wapo hapa visiwani kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi
na kuweza kuwapa matibabu watu wote .
EmoticonEmoticon