Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga (wa kwanza kulia)
akimkabidhi Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC), James Rhombo tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2014 mara baada ya
Shirika hilo na mengine mawili kutangazwa kuwa mwajiri bora wa mwaka
2015 iliyotolewa na Chama Cha Wafanyakazi wa Migodini, Ujenzi, Nishati
na Kazi nyingine (TAMICO). Katikati ni Mwenyekiti wa TAMICO Taifa,
Mbaraka Igangula akishihudia. Katika tuzo hizo jumla ya waajiri 160
walishindanishwa na kupatikana watatu bora ambao ni NHC, Kampuni ya
kuchimba madini ya Geita Gold Mining (GGM) na Wakala wa Ujenzi wa
Barabara Tanzania (Tanroad).
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo
(Kulia) Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Muungano Saguya na Meneja wa
Mawasiliano kwa Umma wa NHC, Yahya Charahani wakiimba wimbo wa
solidarity forever wakati wa hafla hiyo.
Mwenyekiti wa TAMICO Taifa,
Mbaraka Igangula akizungumza katika hafla hiyo wanaoshuhudia ni Naibu wa
Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga na Katibu Mkuu wa Tamico, Hassan
Ameir.
Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Muungano Saguya akiwa ameshikilia tuzo ya
mwajiri bora wa mwaka 2015 huku Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo na Katibu wa Tamico, NHC Iddi
Kitete wakishuhudia.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo akizungumza kutoa shukurani wakati wa hafla hiyo
Picha ya pamoja
Mwenyekiti
wa TAMICO Taifa, Mbaraka Igangula akizungumza katika hafla hiyo
wanaoshuhudia ni Naibu wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga na Katibu
Mkuu wa Tamico, Hassan Ameir.
Naibu
Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga (wa kwanza kulia) akikabidhi
kwa Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),
James Rhombo tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka 2014 mara baada ya Shirika
hilo na mengine mawili kutangazwa kuwa mwajiri bora wa mwaka 2015
iliyotolewa na Chama Cha Wafanyakazi wa Migodini, Ujenzi, Nishati na
Kazi nyingine (TAMICO).
Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa NHC, Muungano Saguya akiwa ameshikilia tuzo ya
mwajiri bora wa mwaka 2015 huku Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika
la Nyumba la Taifa (NHC), James Rhombo na Katibu wa Tamico, NHC Iddi
Kitete wakishuhudia.
…………………………………….
SHIRIKA
la Nyumba la Taifa (NHC) limekuwa miongoni mwa waajiri bora waliopata
tuzo zilizotolewa na Chama cha Wafanyakazi wa Migodini, Ujenzi, Nishati
na Kazi nyingine (TAMICO).
Tuzo hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na chama hicho na kukabidhiwa na Naibu wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga.
Katika
tuzo hizo jumla ya waajiri 160 walishindanishwa na kupatikana watatu
bora ambao ni NHC, Kampuni ya kuchimba madini ya Geita Gold Mining (GGM)
na Wakala wa Ujenzi wa Barabara Tanzania (Tanroad).
Mwenyekiti
wa Tamico Taifa, Mbaraka Igangula, alisema tukio hilo limefanyika kwa
mara ya kwanza, waliamua kulibuni kutokana na kwamba siku zote
wanaotunzwa ni wafanyakazi tu.
Igangula
alisema hiyo itasaidia waajiri kujenga uhusiano mwema na wafanyakazi
wao ambapo wakati mwingine huonekana kama paka na panya.
Alitaja
baadhi ya vigezo vilivyotumika kuwapata washindi kuwa ni uhusiano mzuri
na wafanyakazi, kutekeleza mikataba ya kazi, kuwepo kwa mabaraza,
kushiriki kutoa michango ya kijamii na utekelezaji wa mikataba ya
Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Mwenyekiti
huyo alisema matarajio yao katika kutoa tuzo hizo ni kuwa chachu ya
utekelezaji wa mikataba ya kazi na mazingira wezeshi na rafiki ya




EmoticonEmoticon