KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AITIKISA CHATO MKOANI GEITA

June 15, 2015

1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasha mtambo wa maji uliojengwa Chato Mlimani kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji utakaohudumia wakazi wa mji huo leo wakati wa ziara yake katika mkoa wa Geita , Kinana anaendelea na ziara hiyo ya kikazi mkoani humo baada ya kumaliza ziara kama hiyo mkoani Kagera jana, Kinana anaendelea  na ziara hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015 na kuhimiza uhai wa chama, kukosoa na kutatua matatizo mbalimbali yanayokabili wananchi kwa maisha na maendeleo yao kwa ujumla akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSI CHA FULLSHANGWE-CHATO-GEITA)
2
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na Mkuu wa wilaya ya Chato Rodrick Mpogolo kulia wakipiga makofi mara baada ya kuwashwa rasmi kwa mtambo huo.
3
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Rodrick Mpogolo Mkuu wa wilaya ya Chato na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi pamoja na viongozi wa CCM wilaya ya Chato wakipunga mikono na wanaCCM mbalimbali katika picha ya pamoja.
4
Baadhi ya wananchi wakigombea kupanda gari kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chato.
5
Baadhi ya akina mama wakiwa na ndoo zao tayari kwa kuchota maji mara baada ya kuzindua rasmi mtambo wa maji Chato Kilimani ambao utahudumia wakazi wa mjini Chato na baadhi ya vijiji.
6
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Paulina Sabinati mara baada ya uzinduzi wa mradi huo.
7
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na  Mkuu wa wilaya ya Chato Ndugu Rodrick Mpogole, viongozi wa CCM wilaya ya Chato pamija na mafundi wa Tanesco akishiriki kutandaza waya za umeme katika mradi wa umeme vijijini REA katika kijiji cha Mkungo.
8 9
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukisimama baada ya wananchi wa kijiji cha Mkaurugusi wilayani Chato wakati akielekea kijiji cha Ihanga.
10
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma mabango ya wananchi waliosimamisha msafara wake wakiomba awasaidia kufanikisha mpango wa kuwawekea umeme katika kijiji chao cha Makurugusi ambacho laini ya umeme kuelekea kijiji cha jirani imepitia.
11
Mwakilishi wa wananchi hao wa kijiji cha Makurugusi Bw. Shampinga David akielezea masikitiko ya wananchi hao kutokana na mpango wa umeme vijijini kupita kijiji chao bila kuwawekea umeme huo Bw. Shampinga amemuomba Kinana kuhakikisha anawasaidia na wao wanapata umeme katika kijiji chao.
12
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi hao.
13
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana tano na wananchi hao mara baada ya kuwaahidi kuongea na Waziri wa Nishati na Madini ili kijiji hicho kiwekewe umeme vijiji  REA ambapo wanakijiji hao walijawa na furaha mara baada ya kusikia kauli hiyo kutoka kwa kiongozi huyo wa juu wa CCM.
14
Baadhi ya wananchi wakiwa wamepanda kwenye pikipiki wakielekea kwenye mkutano wa Kinana katika kijiji cha Ihanga ambako alishiriki katika ujenzi wa nyumba ya daktari.
15
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ngoma mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Ihanga.
16
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa nyumba ya daktari katika kijiji cha Ihanga wilayani Chato.
17
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi  na Uenezi akipungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara mjini Chato.
18
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chato.
19
Kwaya ikiimba wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM mjini Chato alipowasili katika mkutano wa hadhara.
20
Wananchi wakinyanyua mikono yao juu juu kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
21
Mkuu wa wilaya ya Chato Ndugu Rodrick Mpogolo akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Chato.
22
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
23
Baadhi ya wananchi wakiwa juu ya magari wakifuatilia hotuba za viongozi mbalimbali katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika mjini Chato mkoani Geita leo.
24
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia mkutano wa hadhara mjini Chato.
25
Nape akisisitiza jambo wakati akihutubia mkutano huo.
26
Umati wa wananchi ukiwa katika mkutano huo.
27
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano huo.
28 29 30 31
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo katika mkutano huo.
32
Baadhi ya wananchi wakirejea nyumbani mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »