Balozi wa Ireland nchini Tanzania
Bi Fionnuala Gilsenan akisaini kitabu cha wageni alipomtembelea Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto) ofisini
kwake leo jijini Dar es salam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiongea na mgeni wake Balozi wa
Ireland nchini Tanzania Bi Fionnuala Gilsenan (kulia) leo jijini Dar es
salam. Kushoto ni Kamishna wa Ardhi nchini Dkt. Moses Kusiluka.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania
Bi Fionnuala Gilsenan akisisitiza jambo wakati alipomtembelea Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi (kushoto) ofisini
kwake leo jijini Dar es salam.
Balozi wa Ireland nchini Tanzania
Bi Fionnuala Gilsenan akiwaonesha Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi William Lukuvi (katikati) na Kamishna wa Ardhi nchini Dkt.
Moses Kusiluka (wa kwanza kushoto) baadhi ya picha na michoro
inayoonesha namna bora ya matumizi ya ardhi kulingana na matumizi husika
ikiwemo mipango miji na vijiji.
…………………………………………….
Na EleuteriMangi-MAELEZO
Serikali inadhamira yadhati kuboresha huduma ya ardhi
nakuipeleka karibu na wananchi kwa wakati ili iwe na tija kwa maendeleo
endelevu.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi William Lukuvi alipokuwa akiongea na Balozi wa Ireland nchini
Tanzania Bi Fionnuala Gilsenan leo jijini Dra es salam.
Akifafanua kuhusu namna huduma hiyo itakavyopelekwa karibu na
wananchi, Waziri Lukuvi amesemakuwa wizara yake imeanzisha kanda nane
ili kusogeza huduma za ardhi karibu na wananchi badala ya hali
ilivyokuwa zamani ambapo huduma hizi zilitolewa makao makuu ya wizara
hiyo tu yaliyopo jijini Dar es salaam.
“Ili kutoa huduma ya ardhi kwa wakati kwa wananchi, huduma ya
utoaji wa Hatimiliki za ardhi sasa ni kwenye kanda ambazo zinasimamiwa
na Makamishna wa Ardhi Wasaidizi.” Alisema Lukuvi.
Kanda hizo ni kanda ya Dar es salaam inayojumuisha Manispaa za
Ilala, Temeke na Kinondoni, kanda ya Mashariki ambapo makao makuu yake
yapo Morogoro, kanda ya Magharibi makao yake makuu yapo Tabora, kanda ya
Ziwa makao yake makuu yapo Mwanza na kanda ya Kaskazini makao yake
makuu yapo Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kanda nyingine ni pamoja na kanda ya kusini ambayo makao yake
makuu yapo Mtwara, kanda ya Kusini Magharibi makao yake makuu yapo Mbeya
na Kanda ya Kati ambayo makao yake makuu yapo mkoani Dodoma.
Katika kutoa huduma yenye ubora kwa wananchi kwa wakati,
Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri wataongeza watumishi wakada za
wapimaardhi, wapangaji wa miji na vijiji pamoja na wathaminia mbao
watafanyakazi kwa pamoja kwenye kanda husika ambapo huduma ya ardhi
itakuwa karibu zaidi na wananchi.
Naye Balozi wa Ireland nchini Tanzania Bi Fionnuala Gilsenan
amempongeza Waziri Lukuvi na watendaji wote wa wizara hiyo kwa kuwa
mstari wa mbele katika kutoa huduma haraka na kwa wepesi zaidi kwa jamii
hatua ambayo ni yakupongezwa na kila mpenda maendeleo.
Balozi Bi Gilsenan alisema kuwa ardhi nibidhaa muhimu inayoweza
kutumika kwa kutoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo elimu, maji,
barabara, ujenzi wa viwanda na miundo mbinu mingine ili kumfanya
mwananchi kupata huduma yenye tija kwa wakati.
Aidha, kwa upande wake Kamishna wa Ardhi nchini Dkt. Moses
Kusiluka alisema kuwa utoaji wa huduma ya usimamizi wa ardhi umeanza
kuboreshwa kwa kubadili mfumo wa utoaji wa huduma kuwa wa kielekroniki
kutoka mfumo wa kawaida, yaani‘manual’.
Dkt. Kusiluka amesisitiza kuwa mfumo wa kielektroniki utaboresha
sana utoaji wa huduma za ardhi, ikiwa ni pamoja nak uondoa tatizo la
milkipandikizi (double allocation), kuondoa udanganyifu, kuongeza
ufanisi wa watendaji na kuongeza mapato ya Serikali.
EmoticonEmoticon