Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) Bw. Felix Ngamlagosi
(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mkurugenzi wa Umeme kutoka mamlaka hiyo, Anastas Mbawalla .
Mkurugenzi wa Umeme kutoka Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) , Anastas akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari leo kuhusu kitabu cha mikataba ya kuuziana
umeme ambacho alishiki kukiandika. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Bw. Felix
Ngamlagosi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA) Bw. Felix Ngamlagosi
(kushoto) akionesha tuzo ya mdhibiti bora wa mwaka wa nishati
iliyotolewa kwa mamlaka hiyo na Jukwaa la Nishati Afrika wakati
akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi
wa Umeme kutoka mamlaka hiyo, Anastas Mbawalla .
Picha na Salma Ngwilizi –Maelezo.
…………………………………….
Na Magreth Kinabo- maelezo
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma
za Nishati na Maji(EWURA) imebuka mshindi wa mashindano ya Tuzo ya
Mdhibiti Bora wa mwaka wa Nishati ya 2015.
Hayo yalisemwa leo na
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bw. Felix Ngamlagosi wakati akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu tuzo hiyo iliyotolewa na
Jukwaa la Nishati la Afrika.
Tuzo hiyo ambayo ilitolewa Juni
8, mwaka huu kwenye sherehe ya mkutano mkuu wa kila mwaka uliofanyika
Juni 8 hadi 11 mwaka huu Dubai,Umoja wa Falme za Kiarabu.
“Jopo la wataalamu la
wanaofanya kazi kwa kushirikiana na shirika la EnergyNet la
Uingereza lilikaa na kuchagua EWURA kuwa ndio mshindi wa kwanza wa
mwaka 2015 katika kundi la wadhibiti,’’ alisema Ngamlagosi.
Ngamlagosi alisema tuzo hiyo
ni ya mara ya kwanza kutolewa nchini imepatikana baada jopo hilo
kuangalia vigezo vya kufanya kazi vizuri, kutoa maelekezo kwa wadau
kwa ufasaha bila mabadiliko, na kueleweka kwa wadau. Pia mamlaka hiyo
imeandaa kanuni mbalimbali ambazo ni za uzalishaji na uuzaji umeme,
usafirishaji umeme na kusambaza umeme zikiwemo leseni.
Aliongeza kwamba tuzo hiyo
inafanya Tanzania kutambulika kimataifa kama ni nchi yenye taasisi
thabiti ya uhakika ya udhibiti wa sekta ya nishati na maji ambalo ni
jambo muhimu kwa nchi kuendelea kuimarisha wawe
Alisema Tanzania sasa
itashuhudia upatikanaji wa kiwango cha juu cha mitaji ya uwekezaji
kutoka nje ya nchi (FDIs)kwenye sekta za nishati na maji ,ambazo
zitavutia uwekezaji zaidi kwenye sekta zingine kwa kuzingatia
kutegemeana kwa sekta kati ya sekta ya nishati zingine kiuchumi.
Hivyo Tanzania ipata wawekezaji
wa umeme mijini na vijijini kutokana na kuwepo kwa mfumo imara na uwazi
unaoleweka katika sekta hiyo.
Ngamlagosi alizitaja taasisi
zingine zilizoshirikia kwenye shindano hilo ni Mamlaka ya Udhibiti wa
Umeme Cameroon(AESEL) Kamisheni ya Udhibiti wa Umeme na Maji ya
Mali(CREE), ]Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati ya Uganda(ERA)na Kamisheni
ya Udhibiti wa Nishati ya Kenya(ERC).
Aliongeza kuwa Tanzania
ilishiriki kuandika kitabu cha mikataba ya kuuziana umeme, ambapo
Mkurugenzi wa Umeme , Anastas Mbawalla alishiriki pamoja na japo la
wataalamu, ambacho kinatarajiwa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi Julai
mwaka huu
EmoticonEmoticon