| Christian Bella akijimwaga jukwaani. |
Masaa
machache baada ya kukosa kitatanishi tunzo ya wimbo bora wa mwaka
katika Kili Music Awards Christian Bela (King of melodies) alipagawisha
wapenzi wa muziki mjini Tabora alipoporomosha bonge la show akiwa na
kundi zima la Malaika Band. Christian Bela alitarajiwa na wadau wa
muziki nchini kuwa angebeba tunzo hiyo bila ushindani mkubwa kutokana na
wimbo wake wa Nani kama mama ambao aliomshirikisha Ommy Dimpoz
kutamba sana katika vituo vyote vya redio na Runinga hapa nchini, lakini
kama kawaida ya tunzo hizo zinazosimamiwa na BASATA na kudhaminiwa na
kampuni ya utengenezaji bia ya Tanzania TBL zimekuwa zikilalamikiwa kila
mwaka huku waanadaaji wakioneka kuweka pamba mbichi masikioni. Tunzo
hiyo ya wimbo bora wa mwaka ilienda kwa wimbo wa Mwana wa msanii Ali
Kiba. Onesho hilo lilifanyika katika viwanja vya Bwalo la Polisi Tabora.
| Bella akifanya yake jukwaani. |
| Mashabiki wa Malaika Band wakpozi |
| Hapo sasa! |
| Baadhi ya mashabiki wakijmwaga! |
| Music Producer Dula K kulia na msanii Masha Kay kushoto wakiwa na mdau. |
| Wacha wee Benny Ngwasuma akijiachia |
Picha na habari na Mkala Fundikira TBN CENTRAL ZONE
EmoticonEmoticon