Mbunge
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wa pili kushoto na viongozi wa
Halmashauri wakikabidhiana daraja la mto Kitewaka kwa ajili ya
kujengwa kisasa baada ya serikali kukabidhi fedha za ujenzi huo Tsh
miloni 240
Mbunge Filikunjombe akilitazama daraja la mbao la mto Kitewaka ambalo litajengwa kisasa
Wannchi wa kijiji cha Maholong'wa wakimpongeza mbunge Filikunjombe kwa kutimiza ahadi yake
Waumini
wa kanisa la Anglikana Maholong'wa Ludewa wakimkabidhi zawadi mbali
mbali mbunge Filikunjombe baada ya kuwasaidia bati na saruji ya
kutosha kujenga kanisa jipya
Viongozi wa kanisa la Anglikana na wa CCM Ludewa wakiongozana na mbunge Filikunjombe mwenye kofia
Mbunge
Filikunjombe akisaidi kupalilia mahindi katika shamba la mchungaji wa
kanisa la Anglicana Maholong'wa baada ya kufika kusaidia ujenzi wa
kanisa hilo
Mkutano wa mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe na wanakijiji wa Maholong;wa
Mzee wa kanisa la E.A.G.T Maboga Ezekia Mhagama (kulia)akimwombea
dua mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe baada ya kutoa misaada mbali
mbali ya ujenzi na kujitolea kinanda kwa kanisa hilo vyote vikiwa
na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 11 wakati wa mkutano wa hadhara
uliofanyika kijiji cha Maholong'wa
Mkurugenzi Ludewa Bw Waziri akizungumza katika mkutano wa mbunge Filikunjombe |
Wananchi wa Maholong'wa wakimpokea mbunge wao
Na matukiodaimaBlog.
MBUNGE
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe ametimiza ahadi yake ya ujenzi
wa daraja la mto Kitewaka katika kijiji cha Maholong'wa kata hiyo
ya Ludende baada ya serikali kumpatia kiasi cha Tsh milioni 2480
zilizokuwa zikihitajika kwa ajili ya ujezi wa daraja hilo .
Mbali
ya kutimiza ahadi hiyo ya daraja pia amechangia vifaa vya ujenzi
vyeye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 11 kwa ajili ya kusaidia ujenzi
wa nyumba ya mwalimu katika shule ya Msingi Maholong'wa na ujenzi
wa kanisa la Anglikana kijiji cha Maholong'wa kata ya Ludende wilayani
Ludewa mkoani Njombe .
Akizungumza na wananchi
hao leo mbunge Filikunjombe alisema kuwa kuwepo bungeni ni heshima
ya wana Ludewa na kuwa hata vurugu kubwa ambazo amekuwa
akizifanya bungeni si kwa maana nyingine zaidi ya kupigania
maendeleo ya wananchi wake.
Hata
hivyo aliipongeza serikali kuwa kusaidia kutoa fedha hizo kwa
wakati kwa ajili ya kuanza ujenzi hao na kuwa iwapo asingefuatilia
kwa karibu serikalini ama angekuwa wa kulala bungeni yawezekana fedha
kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo zisingetolewa sasa.
“wapo wabunge wengine
ambao kazi yao ni kusinzia tu na wala haulizi swali …..ila huo pia
ndio uwakilishi wake ulipoishia …..mimi silali kule bungeni mimi
ninawatetea na kuwapiganieni kwa kulia nalia na kwenye kugombana
nagombana pia pale kwenye kunyenyekea nanyenyekea….. napenda
kuwaelezeni kuwa kazi ambayo mlinipa kuwawakilisha bungeni naitumia
vema hadi sasa sijakwama kuwatumikia ….nilisema mwanzoni mimi
navurugu bungeni ila ni vurugu za kimaendeleo”
Filikunjombe
alisema kuwa waakati akiomba kuwa mbunge wa Ludewa alitaka
kuwawakilisha bungeni na kushirikiana nao katika shughuli za
kimaendeleo hivyo angekuwa mbunge wa ajabu kama angekuwa mbali na
shughuli za kimaendeleo katika jimbo lake .
Alisema
wakati akigombea ubunge mwaka 2010 aliwaahidi wananchi wa kata la
Ludende kuwajengea daraja la kisasa zaidi katika kijiji cha
Maholong'wa ili kuchochea kasi ya maendeleo katika kata ya Ludende na
kata za jirani ,ahadi ambayo sasa anaitimiza kwa kumpata mkandarasi
atakayejenga daraja hilo kwa Tsh milioni 248 na ujenzi wake utaanza
mara moja baada ya mvua kutulia .
“
"Mimi nataka ujenzi huu uanze mara moja kwani
kama shida wananchi wangu mmetesema sana hivyo sasa nataka iwe
basi matesa na sitapenda kuona Halmashauri inaziweka pesa hizo
pasipo kutumika kwa kazi iliyokusudiwa fedha za ujenzi huu zimetoka
serikalini baada ya kuwabana zaidi"
Alivitja
vifaa hivyo kuwa ni bati 200 na saruji 200 pia kinanda kwa kanisa
la E.A.G.T na vifaa mbali mbali vya michezo pamoja na kuwakodia
usafiri kutoka Dar es Salaam hadi kijijini hapo kwa ajili ya
kusafirisha vifaa hivyo.
Awali
viongozi wa madhehebu ya dini na vyama vya siasa katika kata ya
Ludende wilaya ya Ludewa wamepongeza jitihada kubwa zinazofanywa
na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na kuwa hawahitaji
kubadili tena wabunge kama nguo .
Huku
mwenyewe akidai kuwa yeye si mbunge wa kusinzia bungeni ni
makini katika kuwawakilishi wananchi wake na kuwa ana vurugu sana
bungeni ila vurugu zake ni za kimaendeleo si vinginevyo.
Wakishukuru
mara baada ya kuwakabidhi mkandarasi wa kuanza ujenzi wa daraja
, pamoja na saruji na bati kwa ajili ya kuchangia miradi mbali
mbali ya kimaendeleo katika kata hiyo na ujenzi wa kanisa jipya
ya Anglicana kijiji cha Maholong’wa.
Viongozi
hao akiwemo mzee wa kanisa la E.A.G.T Mboga Bw Ezekia Mhagama na
mkuu wa shule ya msingi Maholong’wa Bw Damas Malihayi walisema
kuwa maendeleo makubwa yanayoendelea kuonekana katika wilaya ya
Ludewa ni jitihada kubwa ambazo zinafanywa na mbunge huyo na hivyo
wao kama viongozi wa dini kazi kubwa ni kuzidi kumwombea afya
njema ili aendelee kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa vipindi vingine
zaidi.
Alisema
mzee huyo wa kanisa la E.A.G.T kuwa matumaini ya wananchi wa
Ludewa yamekuwa makubwa zaidi dhidi ya mbunge wao kutokana na sura
ya Ludewa kwa sasa baada ya mateso ya miaka zaidi ya 50 ya Uhuru
bila kuwepo kwa maendeleo yanayoonekana ila toka alipoingia mbunge
Filikunjombe mwaka 2010 wananchi wa Ludewa ndipo walipata uhuru
wao na kuwa wao wanajiona kama miaka hii mitano toka walipomchagua
mbunge huyo kuwa mbunge wao ndipo wao walipopata uhuru wao.
“Tunatambua
nchi yetu ilipata uhuru mwaka 1961 kwa maeneo mbali mbali ya
nchi wananchi wake kusogezewa huduma mbali mbali zikiwemo
barabara za lami ila sisi Ludewa lami tumeanza kuiona mwaka jana
na kama huku Maholong’wa daraja ambalo ni tegemeo kubwa kwetu
lilikuwa la mbao hadi sasa ambapo mbunge wetu ametusaidia kutafuta
pesa ya kujenga daraja la kisasa na huu ndio uhuru wetu “
Mhagama
alipongeza pia kwa msaada wa saruji na bati za kutosha
kukamilkisha ujenzi wa kanisa la Anglicana na msaada wa kinanda
kwa kanisa lake la E.A.G.T kuwa ni mbunge pekee kusaidia jamii
nzima ya Ludewa pasipo kutazama masuala ya itikadi zao .
Hivyo
allisema kwa wananchi wa Ludewa hawana sababu ya kuendelea
kubadili badili wabunge kwa sasa kwani utendaji kazi wa mbunge
Filikunjombe umewakuna wengi na hivyo kazi kubwa kwao ni kuendelea
kumuunga mkono kwa kumpitisha tena na tena kuwa mbunge wao .
Mkuu
wa shule ya Msingi Maholong’wa Bw Malihayi alisema kuwa kuna haja
ya wana Ludewa kushikamana na kuona hawampotezi mbunge huyo na
badala yake kuzidi kumpa ushirikiano zaidi.
Kwa
upande wake Paschal Kayombo akizungumza kwa niaba ya vijana wa kata
hiyo alisema kuwa kero kubwa ya vijana ilikuwa ni daraja hilo la
mto Maholong’wa ambalo kwa sasa limekwisha patiwa ufumbuzi na
kuwa vijana kwa sasa wanaimani kubwa na utendaji kazi wa mbunge
huyo.
Katibu
mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe Honoratus
Mgaya akiwahutubia wananchi hao alisema kuwa CCM ni chama kizuri
sana ila wanaofanya wananchi kukichukia chama ni baadhi ya viongozi
wakiwemo wabunge ambao wameshindwa kuwatumikia vema wananchi
wao.
Kwani
alisema iwapo kila mbunge atafanya kazi kwa kujituma kama ilivyo
kwa mbunge Filikunjombe uwezekano wa kata ama majimbo kuchukuliwa na
vyama vya upinzani usingekuwepo ila wanaopigia kura wapinzani ni
wana CCM ambao wamechoshwa na uwajibikaji mbovu wa wale
waliowachagua.