TANGA UWASA KUKABIDHI VIFAA VYA UJENZI WA MADARASA KWA SHULE YA SEKONDARI MISALAI NA ZIRAI AMANI MUHEZA

March 16, 2015


MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI TANGA(TANGA UWASAMHANDISI JOSHUA MGEYEKWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU WIKI YA MAJI LEO

              
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maadhimisho ya wiki ya maji

                       NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa)inatarajia kukabidhi vifaa vya ujenzi wa madarasa kwa shule ya sekondari za Misalai na Zirai zilizopo Tarafa ya Amani wilayani Muheza vyenye thamani ya milioni 1,110,00.
KUSHOTO NI KAIMU MENEJA WA HUDUMA KWA WATEJA WA MAMLAKA HIYO,ROGERS MACHAKU NA KULIA NI KAIMU AFISA MAHUSIANO WA MAMLAKA HIYO RAMADHANI NYAMBUKA WAKIFUATILIA KIKAO HICHO CHA WAANDISHI WA HABARI NA MKURUGENZI WA MAMLAKA HIYO

Vifaa hivyo ni kwa kutambua mchano wao mkubwa katika kuhifadhi chanzo cha maji cha Mto Zigi ambapo ili kuwa na Maendeleo endelevu kwa Muheza na Tanga ili kuhakikisha maji yanapatikana kwa muda wote kwa kutunza mazingira.


Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maadhimisho ya wiki ya maji ambapo amesema kuwa mamlaka hiyo itamkabidhi Vifaa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Esterina Kilasi ili avikabidhi kwa wahusika.



WAANDISHI WA HABARI WAKIFUATILIA MKUTANO HUO BAINA YAO NA MKURUGENZI WA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI TANGA(TANGA UWASA),MHANDISI JOSHUA MGEYEKWA LEO
Alisema kuwa kuelekea maadhimisho hayo watafanya mikutano ya hadhara kwa kata sita za Jiji la Tanga ili kueleza shughuli wanazozifanya wateja wao na wajibu kwao ikiwemo kuwafafanulia haki zao kama wateja pamoja na kupata maoni yao katika kuboresha huduma wanazozitoa.

Aidha alisema kuwa katika wiki hiyo watazindua rasmi jengo jipya la huduma kwa wateja katika eneo la Pongwe ikiwa ni pamoja na kuzindua huduma ya malipo ya Ankara za maji kwa Tigo Pesa ambapo inatarajiwa kuzinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Said Magalula.

Ameongeza kuwa sambamba na hilo wataendesha dawati maalumu katika ofisi kuu swahili kwa lengo la kuwahudumia wateja wenye madeni sugu pamoja na kuwapa njia rahisi ya kulipia madeni yao na wale watakaolipa watasamehewa ada ya kutejesha maji katika kipindi cha Machi 16 mwaka 22 mwaka huu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »