Pichani
juu na chini ni baadhi ya majengo yaliyokamilika ya Shule ya msingi
Kakuni yaliyojengwa na Waziri Mkuu Pinda kupitia michango ya wadau wa
maendeleo.
Na Andrew Chale wa modewji blog
Kila
mmoja wetu anatambua mchango mkubwa wa elimu hasa ile inayotolewa
ikiwemo ngazi ya Awali, Msingi, Sekondari na elimu ya juu ikiwemo chuo.
Pia katika hilo ni jamb la msingi sana na la maana hasa unapokumbuka
mahala ulipopatia elimu husika.
Mtandao huu wa Mo dewjii blog
tunapenda kuungana na kumpongeza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa juhudi
zake za dhati kabisa katika kuhakikisha shule yake aliyowahi kusoma hapo
inasaidiwa na kufikia malengo yake.
Waziri
Mkuu alipaata elimu yake katika Shule ya msingi Kakuni. Kwa kusoma hapo
darasa la kwanza hadi la nne. Lakini kwa mapenzi mema na juhudi za
kutaka kuona watoto wa hali ya chini hasa wa wakulima wanapata elimu
bora, kwa juhudi zake binafsi, ameweza kusaidia shule hiyo ikiwemo
kutafuta wafadhili mbalimbali wa kuipiga tafu, akiwa kama Mizengo Pinda.
Ambapo unaweza kusoma kiunganishi hichi hapa cha mtandao ili kusoma
habari hiyo zaidi ya wadau kumuunga Waziri Mkuu Pinda katika kuisaidia
shule ya Kakuni: http://dewjiblog.com/2015/03/11/japan-yachangia-sh-milioni-160-shule-ya-msingi-kakuni/
Mtandao
huu unapongeza juhudi hizo za Waziri Mkuu Mizengo Pinda hivyo pia nawe
ukiwa ni miongoni mwa unayeguswa na maendeleo ya elimu hapa nchini, ni
wakati wa kutembelea shule yako uliosoma awali iwe elimu ya ‘vidudu’
yaani Chekechea/Awali, Shule ya Msingi ama Sekondari basi ni wakati wa
kurejea na kusaidia chochote kile ili kuendeleza Elimu hapa Nchini.
Bila
shaka kama Watanzania tutaiga juhudi hizi za Waziri Mkuu Mizengo Pinda,
bila shaka elimu ya Tanzania itapanda maradufu kwani tumeweza kushuhudia
kwa upande wa juhudi hizo za Mizengo Pinda ikiwemo kushawishi wadau
ikiwemo Serikali ya Japan, kutoa msaada wa dola za Marekani, 90,286,
ambazo ni sawa na Sh. Milioni 160.
Fedha
hizo ni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule ya Awali kwenye Shule ya
Msingi, Kakuni iliyopo kijiji cha Kibaoni, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa
Katavi.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda.
Juhudi
za Mizengo Pinda za kuanzisha wazo hilo la kusaidia kuijenga shule yake
ni kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia
kumfikisha hapo alipo.
Kwani alipata kusoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.
Hivyo,
tunatambua wapo wasomi wengi, wapo wabunge, wapo Mawaziri, wapo
Wakurugenzi na wengine wenye vyeo vikubwa Serikali, sekta binafsi na
waliopo ndani nje ya nchi, shime tujitokeze kwa wingi kwa kila mmoja
kwenda kwenye shule aliyosoma na kuchangia chochote.
Tunatambua sisi tumepata elimu wakati gani na kiwango cha elimu wakati
huo kilikuwaje, hivyo tutakapojitokeza kama alivyofanya Waziri Mkuu
Mizengo Pinda, hii itasaidia kukuza elimu yetu hapa Nchini.
Muonekano
wa majengo yaliyokamili ya shule ya msingi Kakuni alipopata elimu ya
msingi Waziri Mkuu Pinda na kuamua kuijenga upya kwa gharama ya zaidi ya
Shilingi bilioni 1.3/- kutokana na michango ya wadau mbalimbali wa
maendeleo.